Home 2023 January 15 DUNIA HII MBOVU!

DUNIA HII MBOVU!

DUNIA HII MBOVU!

“Ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.” (Wagalatia 1:4)

“Je! Nyakati yetu hii ya neema, ambayo Mtume Paulo ameiita ‘dunia hii mbovu iliyopo sasa’, ni mbaya zaidi kuliko wakati wa Nimrodi au kile kinachoonekana katika Warumi 1:18-32?

Nyakati hii ni mbaya. Kila kipindi au enzi katika historia ya mwanadamu imekuwa mbaya. Kila enzi imeonyesha kwamba moyo wa mwanadamu “ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha” (Yeremia 17:9), ndio kusema wanadamu wamekuwa ni wenye dhambi daima na hivyo ni wenye kumhitaji Bwana. Sidhani kama enzi yetu ni mbaya zaidi kuliko wakati wa Nimrodi au kile kinachoelezwa katika Warumi 1:18-32, bali zinafanana sana. Warumi 1:18-32 inaonekana kuwa kama ni ufafanuzi juu ya nyakati zetu hizi! Mwanadamu habadiliki. Wanadamu wamekuwa waovu, ni waovu, na watakuwa waovu.

Habari za uovu wa wanadamu hazipaswi kumshtua yeyote anayemwamini Kristo. Badala yake, zinapaswa kutukumbusha hitaji la wokovu wa Kristo kwa watu wote, na pia hitaji letu la “kuukomboa wakati, kwa maana zamani hizi ni za uovu” (Waefeso 5:16). Imani katika Kristo huleta maisha mapya na inaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya watu, ili sote tuweze kuishi katika tunda la nuru “katika wema wote na haki na kweli” (Waefeso 5:9).

Mtume Paulo anauita “ulimwengu huu mbovu wa sasa” ili kuweka juu yetu utukufu wa ukombozi wetu kutoka kwa ulimwengu huo kwa njia ya Kristo Yesu na Msalaba Wake. Wagalatia 1:4 inatuonyesha “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa.” Ujuvi wa tumaini hili unatufanya tuitikie kwa shukrani na sifa kwa Mwokozi wetu, kwa kusema “Utukufu una yeye milele na milele, Amina” (Wagalatia 1:5), na “ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao” (2 Wakorintho 5:15).

HAKIKA BWANA NDIYE MUNGU; AMINA.

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *