Home 2023 January 08 BARAKA ZETU ZA ROHONI NI HIZI!

BARAKA ZETU ZA ROHONI NI HIZI!

BARAKA ZETU ZA ROHONI NI HIZI!

Tumeokolewa kwa NEEMA

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Waefeso 2:8-9)

Tumepatanishwa na Mungu

“Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.” (Warumi 5:10)

Tumekombolewa

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” (Waefeso 1:7)

Tumesamehewa Makosa Yote

“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;” (Wakolosai 2:13-14)

Tumetakaswa

“Kwa Kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.” (1 Wakorintho 1:2)

Tumetakatifuzwa

“Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama” (Wakolosai 1:21-22)

Tumefunikwa na Kristo

“Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

Tuna Amani na Mungu

“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (Warumi 5:1)

Tu Mwili Mmoja

“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.” (1 Wakorintho 12:13)

Tumeoshwa

“Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.” (1 Wakorintho 6:11)

Tumekubaliwa

“Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.” (Waefeso 1:6)

Tumekamilishwa

“Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.” (Wakolosai 2:10)

Tumebatizwa Katika Kristo

“Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:3)

Roho Mtakatifu Anaishi Ndani Yetu

“Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” (Warumi 8:9)

Tumetiwa Muhuri

“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.” (Waefeso 1:13-14)

Tumefichwa Pamoja na Kristo

“Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.” (Wakolosai 3:3)

Tumehamishwa Kutoka Katika Giza

“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.” (Wakolosai 1:13-14)

Tumefanywa Kuwa Haki ya Mungu

“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (2 Wakorintho 5:21)

Tumehesabiwa Haki Bure

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.” (Warumi 3:23-24)

Tumeifia Torati

“Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.” (Warumi 7:4)

Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote HIZO za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo (Waefeso 1:3)

Ndugu;

MSHUKURU SANA MUNGU WAKO KWA BARAKA ZOTE HIZO ALIZOKUPA – TENA BURE; NA KAMA BADO UNAONA HAZITOSHI NA AU HAZIFAI, BASI ENDELEA KUTAFUTA BARAKA ZINGINE; UNAZOZIJUA WEWE – LAKINI TAMBUA TU KUWA, NI UNAPOTEZA MUDA NA NGUVU ZAKO!!!

UTUKUFU NA UWEZA UNA YEYE MILELE NA MILELE. AMINA.

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *