Home 2022 December 06 “SIRI”

“SIRI”

“SIRI”

Katika Waefeso 3:1-3 “uwakili wa neema ya Mungu” umeitwa kipekee “siri“. Kimsingi, imeainishwa hivyo kwa sababu kuu mbili:

  1. Ilikuwa “imefichwa tangu mwanzo wa ulimwengu, lakini sasa”, kupitia kwa Mtume Paulo, “imedhihirika” (Warumi 16:25). “Katika vizazi vingine” “hawakujulishwa” (Waefeso 3:5). Badala yake, “tangu zamani zote (kabla ya mwanzo wa ulimwengu)” ilikuwa “imesitirika katika Mungu” (Mstari wa 9), ilikuwa “imefichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, lakini sasa imedhihirishwa (imefunuliwa) kwa watakatifu wake” (Wakolosai 1:26).
  2. Ilikuwa, kwa wakati huo huo, ni ufafanuzi na ni ufunguo kwa habari njema zote za Mungu, yakiwemo yale yote ambayo yalikuwa yametangazwa katika nyakati zilizotangulia. Ilifafanua jinsi ambavyo Habili ​​aliweza kutangazwa kuwa mwadilifu kwa kuleta dhabihu ya mnyama, “Mungu akazishuhudia sadaka zake” (Waebrania 11:4); Jinsi Nuhu alivyoweza kuwa “mrithi wa haki” kwa kuunda safina (Waebrania 11:7); Ilifafanua pia jinsi ambavyo mtu yeyote angeweza kuokolewa chini ya maongozi ya Sheria; na zaidi sana, jinsi ambavyo tunaweza kuokolewa leo kwa neema kwa njia ya imani pekee.

Ndiyo kusema, katika nyaraka za Mtume Paulo, hatuna tu injili – habari njema ya “siri” (Waefeso 3:1-3); Bali pia, tunayo “siri ya Injili” (Waefeso 6:19-20).

Siri hii kuu, iliyofunuliwa na kupitia kwa Mtume Paulo, kwa ufasaa imeitwa jiwe kuu la ufunuo wa kimungu, kwa kuwa inahusu kusudi la umilele la Mungu katika Kristo. Kupitia kwa Mtume Paulo, mkuu wa wenye dhambi waliookolewa kwa neema, Mungu sasa ametujulisha siri hii tukufu (Waefeso 1:9) ili sisi, nasi tuweze kuijulisha siri hiyo kwa wengine (Waefeso 3:9-11).

“Kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Utukufu una Yeye KRISTO, Milele na Milele; AMINA.

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *