Home 2022 December 01 HAKUNA TOFAUTI!

HAKUNA TOFAUTI!

HAKUNA TOFAUTI!

Mara mbili katika Kitabu cha Warumi; sehemu ya kwanza ni katika Warumi 3:22-23, na sehemu ya pili ni katika Warumi 10:12-13; Mungu, kupitia andiko la Mtume Paulo anatumia maneno, “HAKUNA TOFAUTI.”

Mara ya kwanza, maneno hayo yametumika uhusiano na hatia ya mwanadamu – WOTE! Wayahudi wenye kidini, pamoja na watu wa Mataifa wasiomcha Mungu; watu wenye maadili ya kitamaduni, pamoja na washenzi – watu wenye hadhi ya chini, WOTE – wanathibitishwa kuwa na hatia mbele za Mungu.

Katika sura tatu za kwanza za kitabu cha Warumi, mapendeleo yao na wajibu wao unazungumzwa kikamili, na hoja zao pia zinazingatiwa kwa uangalifu. Kisha inakuja hukumu ya kutisha:

“HAKUNA TOFAUTI: KWA MAANA WOTE WAMETENDA DHAMBI NA KUPUNGUKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU.”

Je! Si busara yenye ulazima kwetu sisi sote kuinamisha vichwa vyetu chini kwa aibu na kukiri kwamba hati hiyo ya mashtaka ni ya kweli? Je! hatupaswi kukiri kwamba hukumu hiyo kwetu ni ya haki? Ni kweli kwamba, kunaweza kuwa na tofauti katika asili au kiwango cha dhambi zetu, lakini katika hili hakuna tofauti: kwa kuwa sisi sote tumefanya dhambi. Na Mungu mwenye haki na mtakatifu ni lazima ailaani dhambi.

Ni jambo la faraja, hata hivyo, kuona maneno yanatumika mara ya pili kuhusiana na wokovu. Na hapa tena, Wayahudi wenye kidini pamoja na watu wa Mataifa wasiomcha Mungu wamejumuishwa, lakini wakati huu, tangazo hilo ni tangazo lililojaa uwingi wa neema isiyo kifani!

“KWA MAANA HAKUNA TOFAUTI YA MYAHUDI NA MYUNANI; MAANA YEYE YULE NI BWANA WA WOTE, MWENYE UTAJIRI KWA WOTE WAMWITAO; KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.”

Katika suala la dhambi, Mungu hawezi kuwa na ubaguzi. Hawezi kuwa mpole kwa tabaka fulani au vikundi ambavyo vinaonekana kuwa na faida. Wote wamefanya dhambi, na wote wanapaswa kuhukumiwa.

Lakini Mungu, wala haonyeshi upendeleo katika suala la wokovu pia. Tajiri au mtu wenye maadili ya kitamaduni au mtu wa kidini; Mungu hawapendelewi zaidi ya wengine. Wasiojua kusoma na kuandika au wasio na maadili nao hawajatengwa. Sheria inawahukumu wote, lakini Kristo Yesu alikufa msalabani ili kuwaokoa wote, ili sisi “tuhesabiwe haki bure kwa neema yake.”

Je! Wewe rafiki yangu, umeokoka? Je, uko sawasawa na mapenzi ya Mungu? Kumbuka; Kamwe huwezi kutumaini kukubaliwa Naye, ikiwa unamwendea Yeye kwa sifa zako wewe mwenyewe, lakini ikiwa unamwendea kwa sifa za Yeye aliyebeba dhambi zako, huwezi kuachwa:

“KWA MAANA YEYE YULE NI BWANA WA WOTE, MWENYE UTAJIRI KWA WOTE WAMWITAO; KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.”

Utukufu una Yeye KRISTO, Milele na Milele; AMINA.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *