Home 2022 July 01 Dhambi Inasamewehaje?

Dhambi Inasamewehaje?

Dhambi Inasamewehaje?

Takribani miaka elfu tatu hivi iliyopita, na karibu miaka elfu moja kabla ya Kristo, Mtunga Zaburi alisema hivi:

“Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.” (Zaburi 130:3-4)

Mzaburi huyu hakueleza, hata hivyo, ni kwa msingi gani Mungu mwenye haki na mtakatifu angeweza kumsamehe mtu mwenye dhambi, mtu mwenye hatia! Hili lilipaswa kutangazwa, miaka elfu moja baadaye, na mtu mmoja aliyeitwa Sauli wa Tarso; anayejulikana kama Mtume Paulo, ambaye wakati fulani alikuwa “mtukanaji, muuaji, mtesaji na mdhalimu”; alikuwa ni “mkuu” wa wenye dhambi, lakini alisamehewa na kuokolewa kwa neema ya Mungu isiyo na kikomo (1 Timotheo 1:12-15).

Akimhubiri Kristo huko Antiokia, katika jimbo la Pisidia, Mtume Paulo alisema maneno haya:

“Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa KWA HUYO MNAHUBIRIWA MSAMAHA WA DHAMBI; NA KWA YEYE KILA AMWAMINIYE HUHESABIWA HAKI KATIKA MAMBO YALE YOTE ASIYOWEZA KUHESABIWA HAKI KWA TORATI YA MUSA.” (Matendo 13:38-39)

Lakini hata hili bado halijajibu swali letu kikamilifu, kwa maana bado tunapaswa kujiuliza:

Ni kwa msingi upi/gani Mungu mwenye haki na mtakatifu, anasamehe dhambi za wanadamu kupitia “KWA HUYO”?

Jibu lake ni kwamba:

Kwa msingi wa malipo yaliyofanyika “KWA HUYO” kwa ajili ya dhambi zetu juu ya msalaba wa Kalvari…

Kwa sababu hiyo, ndio maana Mtume Paulo aliwaandikia Warumi, akiwaeleza jinsi walivyo/tulivyo kwa sababu ya “HUYO”…

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, KWA NJIA YA UKOMBOZI ULIO KATIKA KRISTO YESU” (Warumi 3:23-24).

Hivyo, TUNAMSHUKURU sana MUNGU, kupitia kazi kamilifu ya UKOMBOZI ya Kristo YESU, ambayo inamwezesha kila mwenye dhambi, anayehitaji MSAMAHA WA DHAMBI aweze kusamehewa, kwa kuwa:

“Katika YEYE HUYO, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, MASAMAHA YA DHAMBI, SAWASAWA NA WINGI WA NEEMA YAKE.” (Waefeso 1:7)

Utukufu Una Yeye KRISTO, Milele na Milele; AMINA.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *