Home 2022 May 15 Mtume wa Neema

Mtume wa Neema

Mtume wa Neema

Kuongoka kwa Sauli wa Tarso lilikuwa ni tukio la kushangaza. Sauli alilichukia sana jina la Kristo Yesu. Alimkufuru na kusababisha wengine kuteswa ili kuwashurutisha kulitukana jina hilo takatifu. Aliongoza taifa lake na ulimwengu katika uasi dhidi ya Kristo aliyefufuka, Kristo aliyetukuzwa – ulimwengu ambao tayari ulikuwa umemkataa na kumsulubisha Yesu kama mtu wa hali ya chini sana.

Lakini Sauli alipokuwa akielekea Dameski, huku akiwa bado “akitoa vitisho na mauaji dhidi ya wanafunzi wa Bwana” (Matendo 9:1), Mungu alifanya jambo la ajabu – alifanya tendo la REHEMA na NEEMA! Badala ya kumkandamiza/kumwangamiza kiongozi huyo wa uasi wa ulimwengu, Alimuokoa. Kristo alipasua mbingu, ili aweze kusema maneno ya huruma kwa adui wake mkuu zaidi duniani. Matokeo yake, roho ya uasi ya Sauli ilivunjwa na kwa dakika moja yule mtesaji asiye na huruma akawa mtulivu, na kugeuka kuwa mfuasi aliyejitolea wa Kristo.

Zaidi ya hayo, Sauli wa Tarso, mtesaji, akawa Paulo Mtume. Kwake yeye, Bwana aliyetukuzwa, alikabidhi “maongozi ya neema ya Mungu” (Waefeso 3:2) na “injili ya neema ya Mungu” (Matendo 20:24). Sasa akaenda kila mahali akitangaza neema ya Mungu, akiwaambia wanadamu jinsi Mungu alivyowapenda, jinsi Kristo alivyokuja ulimwenguni na kwenda Kalvari kulipa deni la dhambi la mwanadamu ili wenye dhambi wanaoamini wapate kuokolewa.

“Injili ya neema ya Mungu,” inayopatikana katika nyaraka za Paulo pekee, haimlaumu mtu yeyote kwa kifo cha Kristo. Badala yake, inawasilisha msalaba kama habari njema. Inatangaza kwamba “kwa damu yake tuna ukombozi, masamaha ya dhambi sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7). Inasema kwamba “Mungu amewafunga wote katika kutokuamini ili awarehemu wote” (Warumi 11:32) na kwamba “dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi” (Warumi 5:20).

Hivyo mwenye dhambi mbaya zaidi anaweza kuamini na kufurahia ufahamu wa dhambi zilizosamehewa…

Utukufu na Wema na Uweza Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *