Home 2022 April 15 Jeneza la Sheria!

Jeneza la Sheria!

Jeneza la Sheria!

Mara tu baada ya muda mchache kupita baada ya Musa kupewa Sheria pale Sinai, Mungu aliamuru iwekwe kwenye jeneza. Hivyo ndivyo ilivyo; Huo ndio ukweli ulivyo – jeneza! Sababu yake ni kwamba agano la Musa lilinena wazi hivi:

“Sasa basi IKIWA MTAITII SAUTI YANGU KWELI KWELI, na kulishika agano langu, HAPO NDIPO mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu.” (Kutoka 19:5)

Israeli, bila kuacha shaka yoyote, hawakutii sauti ya Mungu ‘kweli kweli’; bali kinyume chake, walivunja Sheria hiyo hata kabla ya Musa mwenyewe hajashuka kutoka Mlimani Sinai. Ilikuwa ni kwa sababu ya jambo hili, ambalo lilimfanya Mungu, kwa neema yake, aamuru kuwa:

“Nao na watafanye sanduku…” (Kutoka 25:10)

Neno hili “sanduku” – אֲרוֹן (a.ron) ‘ark’ – limetafsiriwa “jeneza” katika mstari wa mwisho wa kitabu cha Mwanzo (Mwanzo 50:26) na hiyo ndiyo maana yake rahisi. Lakini kwa nini Mungu aliamuru jeneza kuwa kifaa cha kwanza kabisa cha hema la kukutania? Jibu lake ni kwa ajili ya: Kuweka Sheria ndani yake! Jisomee mwenyewe hapa:

“Kisha tia ndani ya JENEZA huo ushuhuda nitakaokupa. Weka KITI CHA REHEMA juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku.” (Mstari wa 16, 21)

Kama Mungu hangeweka agano la Sheria kwenye jeneza na kukutana na watu wake kutoka kwenye “kiti cha rehema”, hapangekuwa na hata mmoja wao ambaye angeweza kuokolewa!

Aina hii ya Agano la Kale lina funzo kubwa kwetu hivi leo, kwani kama Mungu angetutendea kulingana (sawasawa) na matendo yetu (kazi zetu) hapatakuwa na hata mmoja wetu ambaye ataweza kuokolewa, lakini “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu”; akitimiza kwa ajili yetu mahitaji (madai) ya haki ya Sheria iliyovunjwa, ili tupate (tuweze) kuokolewa kwa neema kwa njia ya imani katika kazi Yake ya ukombozi.

Wakolosai 2:14 inasema kuhusu ile “hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu,” ambayo Bwana wetu, kwa kifo chake, “akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani,” na Warumi 7:6 inafafanua zaidi kuwa:

“Bali sasa TUMEFUNGULIWA KATIKA TORATI, TUMEIFIA hali ile iliyotupinga, ILI SISI TUPATE KUTUMIKA KATIKA HALI MPYA YA ROHO, si katika hali ya zamani, ya andiko.”

Hivyo waaminio wote katika Kristo wanaokolewa “kwa neema…, kwa imani…; si kwa sababu ya matendo yao mema” BALI “ili waweze kutenda matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatayarisha ili tuenende nayo” (Waefeso 2:8-10):

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *