Home 2022 March 18 Wakati Ulikuwa Umewadia!

Wakati Ulikuwa Umewadia!

Wakati Ulikuwa Umewadia!

“Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu” (Tito 1:1-3)

Katika Sheria ya Musa, Mungu aliwaahidi watu wa Israeli kwamba wangeweza “kuishi” (Walawi 18:5) – kuishi milele – ikiwa tu wangezishika amri zake. Tunajua hivyo ndivyo Mambo ya Walawi 18:5 ilimaanisha kwa sababu Bwana alinukuu mstari huo kwa ‘mtu’ aliyekuwa akitafuta uzima wa milele katika Luka 10:25-28:

“Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.”

Lakini Mungu alituahidi sisi watu wa Mataifa uzima wa milele kabla ya Sheria ya Musa, yaani – hata “kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu.” Lakini tofauti na ahadi ya uzima wa milele Mungu Aliyowapa Wayahudi katika Sheria hiyo, Hakuifunua ahadi yake hiyo, kwetu sisi watu wa Mataifa, kwa maelfu ya miaka! Akizungumzia ahadi hiyo katika Tito 1:2, Mtume Paulo aliongeza kwa kusema maneno haya,

“…akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi …” (Tito 1:3)

Hatimaye, wakati Mungu alipoamua kuifunua ahadi ya kuwapa watu wa Mataifa uzima wa milele, alimchagua mtu mmoja; Mtume Paulo kuitangaza habari hiyo. Wakati ufaao wa Mungu ulikuwa umewadia wa kuifichua ahadi yake hiyo, iliyofichwa tangu milele!

Lakini Je! Maneno haya, ‘wakati unaofaa’, yanamaanisha nini? Hilo ni swali la msingi! Msemo huu ‘wakati unaofaa’ ulitumika wakati baadhi ya Wayahudi wasioamini walipokuwa wakiwatesa baadhi ya Wayahudi walioamini katika Israeli, na Wayahudi hao walioamini walikuwa wakijiuliza ni kwa muda gani Mungu angeruhusu jambo hili liendelee bila Yeye kuingilia kati! Mungu akawajibu,

“Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa” (Kumbukumbu la Torati 32:35-36)

Mungu aliwaambia waamini hao walioteswa, kana kwamba ni kweli, “Nitawahukumu ‘makafiri’ (wale wasioamini) miongoni mwa watu Wangu kwa wakati ufaao, na wakati huo utawadia pale nitakapoona kwamba nyie watumishi Wangu (ninyi mnaoniamini) hamna uwezo wa kujiokoa kutoka kwenye mateso yao.” Kwa hiyo, maneno ‘wakati unaofaa’, hurejelea wakati ambapo Mungu huwatazama wanadamu na kuona kwamba “nguvu zao zimetoweka” – na “hawana uwezo tena wa kujitetea”!

Hili sasa, litatusaidia kuyaelewa, maneno hayo yakionekana:

“Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.” (Warumi 5:6)

Wayahudi walikuwa wameapa kwamba wangeweza kuishika Sheria (Kutoka 24:7), lakini kwa kipindi cha muda wa takribani miaka 1500 hivi  iliyofuatia, walionyesha kwamba hawakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Na walipoonyesha kwamba “hawakuwa na nguvu” za kuitunza Sheria hiyo, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.

Lakini kwa kadiri mtu yeyote ajuavyo, Kristo alikufa tu kwa ajili ya Wayahudi wasiomcha Mungu, watu wa Isaya (Isaya 53:8). Alikufa tu “ili kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mathayo 20:28) – “wengi” katika Israeli – kwa sababu hayo ndiyo yalikuwa ‘mambo yote’ ambayo Mungu alikuwa ameyafunua hadi wakati huo.

Ni mpaka pale unapoyafikia maandiko ya Paulo ndipo unaposoma kwamba “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.” (1 Timotheo 2:5-6). Na jambo lililofanya hilo kuwa ni ‘wakati unaofaa’ kwa Paulo kushuhudia hili ni kwamba hapo ndipo ilipodhihirika kwamba watu wa Mataifa nao hawakuwa na nguvu za kujiokoa pia!

Kama huna uhakika wa nini ninamaanisha katika hilo, tambua kwamba kipindi kile, kama mtu wa Mataifa alitaka kuokolewa; ilimpasa mmataifa huyo kuwa Myahudi kwanza – Myahudi kweli kweli, Myahudi aliyeamini – aliyemwamini Mungu wa Wayahudi. Kwa watu hao wa Mataifa, wokovu ulipatikana “katika mabaki” katika Yerusalemu (Yoeli 2:32). Hiyo ndiyo sababu Bwana aliwatuma mabaki ya mitume 12 kwenda kwa watu wa Mataifa katika “mataifa yote” (Luka 24:47).

Lakini wale Thenashara waliambiwa waipeleke injili kwa mataifa yote “kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47). Wayahudi katika Yerusalemu walipompiga kwa mawe Stefano badala ya kulipeleka “neno la Bwana kutoka Yerusalemu” (Isaya 2:3), ilionekana kana kwamba watu wa Mataifa wangebaki bila nguvu za kuokolewa.

Hapo ndipo Mungu alipomwinua Paulo ili awashuhudie hao watu wa Mataifa kwamba Mataifa sasa hawapaswi kuwa Wayahudi kwanza ili kupata uzima wa milele ambao Mungu aliwaahidi Israeli katika Sheria, kwa kuwa Mungu alikwisha kuwaahidia (wao watu wa Mataifa) uzima wa milele kabla ya ulimwengu kuanza!

Je! Huu si wakati muafaka kuipokea “ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu” (2 Timotheo 1:1) kwa kuamini kwamba Kristo Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka tena (1 Wakorintho 15:1-4) ili tuwe na uzima wa milele? KWA SABABU HATUNA NGUVU YOYOTE YA KUJIOKOA…

Utukufu na Wema na Uweza Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *