Home 2022 March 06 Kuukabili Ukweli!

Kuukabili Ukweli!

Kuukabili Ukweli!

Waraka wa Paulo kwa Warumi, Sura ya Kwanza na ya Pili, inatoa taswira mbaya ya jamii ya kibinadamu; lakini ukiubali ukweli huo ulioandikwa, utakuwa umechukua hatua ya kwanza ya wokovu! Kwa asili yetu, tumekuwa tukisitasita kuzikabili dhambi zetu; ingawa ingekuwa ni vyema zaidi kama tungezikubali dhambi zetu hizo.

Ikiwa mtu ana dalili za mapema za kansa, na daktari wake akaendelea kumficha ukweli huo, mtu huyo atakuja kufa kwa kansa. Daktari mzuri na mwenye hekima atasema: “Una dalili za kansa na tunapaswa kuanza kufanya matibabu bila kukawia zaidi.”

Hivyo Mungu wetu, katika Neno Lake, ametuambia kwa uwazi kabisa kuhusu hali yetu hiyo ya dhambi; sio kwa nia ya kutuhukumu, bali ili aweze kutuokoa kutoka kwayo.

Hapa ndipo falsafa nyingi za kibinadamu ‘zinapogongana’, uso kwa uso na Biblia. Falsafa hizo hufunga macho yake juu ya asili ya dhambi ya mwanadamu. Wanaamini kwamba, mwanadamu kwa asili yake, ni mtu mwema; ingawa uthibitisho mwingi wa Kibiblia unatoa ushahidi kwamba mwanadamu ni mwenye dhambi kwa asili yake. Kwa hiyo, falsafa hizo za kibinadamu hazitoi jawabu la jinsi ya kutoka kwenye dhambi hizo na adhabu yake ya haki. Ni “injili ya neema ya Mungu” pekee ndiyo inafanya hivyo.

Biblia inasema haya kuwahusu wanadamu wote: “Wote wamefanya dhambi” (Warumi 3:23), na kwa kila mtu binafsi inasema hivi: “Huna udhuru” (Warumi 2:1). Lakini Biblia hiyo hiyo pia inasema hivi: “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Wakorintho 15:3), na “Tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7).

Utukufu na Wema na Uweza Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *