Home 2022 February 20 Kushindwa Mara Saba!

Kushindwa Mara Saba!

Kushindwa Mara Saba!

Pamoja na mwelekeo wa asili wa mwanadamu wa kujisifu, historia imethibitisha tena na tena kwamba yeye ni mtu asiyefaa kwa lolote, na ni mtu anayemhitaji sana Mungu na Neema Yake…

Enzi ya Kutokuwa na Hatia ilifungwa kwa mwanadamu kumwasi Muumba wake na kuwa kiumbe aliyeanguka na mwenye dhambi (Warumi 5:12).

Enzi ya Dhamiri ilifunguliwa kwa mauaji moja (Mwanzo 4:8) na kabla ya enzi nyingine kuingizwa “dunia ilijaa jeuri” (Mwanzo 6:11).

Kisha ikaja Serikali ya Kibinadamu, lakini mtawala wa kwanza wa ulimwengu ‘alijivua nguo’ mwenyewe kupitia ulevi (Mwanzo 9:20-21). Si ajabu, tunaona kwamba, kipindi kifupi tu baadae jamii hiyo inalewa kwa ukengeufu wake na hivyo kumfanya Mungu avuruge lugha yao pale Babeli (Mwanzo 11:4, 7-8).

Enzi ya Ahadi ilifuata, huku Ibrahimu akishindwa kuingia katika nchi ya ahadi kwa kutokuamini (Mwanzo 11:31-12:3). Ilifungwa kwa Israeli, uzao wake, nao kushindwa kuingia katika nchi ya ahadi kwa kutokuamini (Waebrania 3:19).

Enzi ya Sheria ilianza na Israeli kuabudu ndama wa dhahabu kabla hata Musa hajashuka kutoka Sinai. Si ajabu, iliisha kwa Israeli kumkataa Kristo!

Enzi ya Neema ilianza na Mtume Paulo, balozi wa Mungu wa upendo na neema, ambaye aliteswa na kufungwa (Waefeso 6:20). Hii ilionyesha mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu na neema Yake. Itahitimishwa wakati mwanadamu anaendelea, bila kukoma, katika dhambi zake badala ya kukubali neema ya ukombozi kupitia Kristo (2 Wakorintho 4:4; 2 Timotheo 3:1-5).

Ufalme wa Kristo, ambao utafuata wakati huu wa sasa, utaanza na Bwana wetu kukemea mataifa yenye nguvu (Mika 4:3) na utafunga na makutano, ambao kwa muda walikuwa wameonyesha utii wa kulazimishwa, wakimfuata Shetani (Ufunuo 20:7-9).

Haya yote yanaonyesha jinsi mwanadamu anavyomhitaji Mungu na wokovu wake kupitia Bwana wetu Yesu Kristo! “Wote wamefanya dhambi” (Warumi 3:23) lakini, tunamshukuru Mungu kwamba: “Kila mtu atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa” (Warumi 10:13). Ingawa, tumezungukwa na dhambi na uasi, watu wengi katika historia wameita na wameokolewa. Wewe unangoja NINI…???

Sifa na Uweza na Ukuu Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *