LO-AMI

LO-AMI

Tunaishi katika kipindi cha wakati kinachoitwa Lo-Ami kwa Israeli, kwa maana Mungu sasa anashughulika na mataifa yote kwa usawa…

Mwishoni mwa Matendo (28:28), Mungu alizindua Lo-Ami kwa watu wake, Israeli wa Biblia, kwamba “Si watu wangu, na mimi si Mungu wenu”, na hivyo kutimiza unabii wa Hosea. Hii lilianza takribani miaka 2,000 iliyopita (siku 2), kipindi cha mabano, wakati saa ya Mungu na Israeli iliposimama na kuanza mwanzo wa wakati mwingine ambapo Mungu anashughulika na watu wote sawasawa – kuhusu neema yake na wokovu.

Miaka ya Lo-Ami haijajumuishwa katika saa ya kinabii ya Mungu na Israeli. Israeli na ufalme wao wa Mbinguni wako katika hali ya kutokuwepo (kuhairishwa) kwa muda hadi hapo Mwili wa Kristo utakapojazwa kikamilifu na wakati huu wa sasa utimilike.

Nini kinabaki??? Miaka ambayo Mungu ataikomboa Israeli, na kuanzisha tena maagano yake na Israeli, na kurejesha tena ufalme kwa Israeli na Kristo atakuwa ndiye Mfalme wao (Ufalme wa Milenia).

Kwa sababu, Mungu bado hajamalizana na Israeli…

Hosea 1:9

“Bwana akasema, Mwite jina lake Lo-ami kwa maana ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa MUNGU wenu.”

Hosea 3:4

“Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago

Hosea 6:2

“Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake”

Isaya 54:7

“Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya

Isaya 54:8

“Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako.”

Sifa na Uweza na Ukuu Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *