Home 2022 January 29 Uasi Dhidi ya Mamlaka ya Paulo

Uasi Dhidi ya Mamlaka ya Paulo

Uasi Dhidi ya Mamlaka ya Paulo

Moja ya sababu kuu kwa nini watu wengi, waaminifu wa kidini, wameachwa katika mashaka na kutokuwa na uhakika kuhusu wokovu wao ni kwa sababu Kanisa ‘lililopangwa’ limeasi dhidi ya ufunuo tofauti na utume mwingine, muhimu zaidi kutoka kwa Mungu; kwetu sisi tunaoishi katika enzi hii ya sasa ya majira ya Neema ya Mungu. Ufunuo huu unapatikana katika maneno yaliyoongozwa (yaliyovuviwa) na Roho Mtakatifu, kupitia kwa Mtume wa majira haya, katika Warumi 11:13:

Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu.

Watu wengi, kwa kujua au kutokujua, ‘wanayapunguza’ yale ambayo Neno la Mungu LIMEYAKUZA hapa. Wanasisitiza kumfuata Mtume Petro badala ya Mtume Paulo, wakishindwa kutambua kwamba mamlaka ya Petro yalihusu ufalme wa Yesu Kristo uliokataliwa sasa hapa duniani, juu ya taifa la Israeli na mataifa mengine. Bwana wetu aliwaambia Mitume wake kumi na wawili, maneno haya (na ieleweke hapa kwamba, Yesu Kristo hakuwahi kusema uwongo wala kukosea na maneno yake yote ni amini):

“Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, NINYI NANYI MTAKETI KATIKA VITI KUMI NA VIWILI, MKIWAHUKUMU KABILA KUMI NA MBILI ZA ISRAELI” (Mathayo 19:28)

Kwa hakika hakuna makabila kumi na mawili katika Kanisa leo, wala hakuna mpango wowote, mahususi au uliodokezwa, ulioandaliwa na Bwana wetu kwa ajili ya “mlolongo wa kitume.” Fundisho hili la ‘kulazimishwa’ limejengwa juu ya dhana isiyo ya kimaandiko kwamba Kanisa leo ni ufalme ambao Kristo alianzisha alipokuwa hapa duniani, na kwamba huduma yetu leo ​​ni uendelezaji tu wa yale ambayo wale mitume kumi na wawili waliyaanzisha.

Ukweli ni kwamba, huduma ya wale mitume kumi na wawili ilisimamishwa kwa kukataliwa kwa Mfalme na Ufalme Wake na kwamba mitume wenyewe hatimaye walikubali kukabidhi huduma yao iliyopendekezwa ya kwenda kwa watu wa Mataifa kwa Mtume Paulo, mtume yule mwingine, ambaye alikuwa amekabidhiwa “Injili ya Neema ya Mungu” (Soma kwa umakini, Matendo 20:24 na Wagalatia 2:2-9).

Laiti kama, umati huu wa watu wa kidini uliochanganyikiwa, ungeweza kuona na kutambua tu ni wakati gani hasa Israeli ilipoungana na Mataifa katika kumwasi Mungu; wakati ule dhambi ya ulimwengu ilipokuwa imepanda na kufikia kiwango cha juu sana na yote yalikuwa tayari kwa hukumu; Mungu alipoufunua “utajiri wa wingi wa neema yake” kwa kumwokoa Sauli, mkuu wa wakosefu, na kumtuma kuwa mhubiri na kielelezo hai cha ukubwa usiopimika wa neema yake…!

Hivyo, Paulo anaandika:

“Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; ili kwamba, KAMA VILE DHAMBI ILIVYOTAWALA KATIKA MAUTI, VIVYO HIVYO KWA NJIA YA HAKI NEEMA ITAWALE hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.” (Warumi 5:20-21)

Sifa na Uweza na Ukuu Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *