Home 2022 January 23 Yaliyopungua ya Mateso ya Kristo

Yaliyopungua ya Mateso ya Kristo

Yaliyopungua ya Mateso ya Kristo

Wakolosai 1:24

Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake”

ANGALIZO:

Ipo tofauti katika ya:

Yale yaliyopungua “YA” mateso ya Kristo; na

Yale yaliyopungua “KATIKA” mateso ya Kristo; kama LUGHA ina maana!

 

Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu – Kwa ajili yenu kama sehemu ya ulimwengu wa watu wa Mataifa. Mateso yake hayakuwa kwa ajili ya Wakolosai peke yake, bali Paulo alijiona kuwa anateseka kwa sababu ya kazi yake ya kuwahubiria injili wapagani (Mataifa) kwa ujumla wake. Majaribu yake kule Rumi (na mahala pengine kabla ya Rumi) yalikuwa yamemjia kwa sababu alikuwa amesimamia kutangaza kwamba ukuta wa farakano kati ya Wayahudi na Mataifa ulikuwa umebomolewa (Waefeso 2:11-22), na kwamba injili ilipaswa sasa kuhubiriwa bila ubaguzi kwa wanadamu wote.

Tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo – Yale ambayo siwezi kuyafikia; mateso ambayo Kristo aliyastahimili kwa ajili ya kanisa! Katika hili, Mtume Paulo anaonekana kumaanisha kwamba alikuwa bado hajateseka sana kama vile Kristo alivyoteseka na ingawa alikuwa ameteseka sana, lakini kulikuwa na mengi ambayo yalikosekana ili kumfanya awe sawa na Kristo Mwokozi katika jambo hilo.

Anachosema hapa kinatokana na tamanio kuu la roho yake – kanuni kuu ya maisha yake – kuwa sawa na Kristo; sawasawa katika tabia ya kimaadili, katika mateso, na katika hatima (Wafilipi 3:10). Akiwa na hamu hii kubwa, alikuwa ameongozwa kufuata njia ya maisha ambayo ilimpeleka katika majaribu yanayofanana sana na yale ambayo Kristo mwenyewe aliyavumilia; na, kwa haraka iwezekanavyo, alikuwa akiyapitia (akiyajaza) yale ambayo yalikuwa yamekosekana (kwake yeye).

Ifahamike hapa kuwa, Paulo hamaanishi kwamba kulikuwa na kitu chochote kilichopungua au kulikuwa na upungufu katika mateso ambayo Kristo aliyavumilia katika kufanya kwake upatanisho ambayo yalipaswa kuongezwa (kusaidiwa) na wafuasi wake, ili matokeo mema ya kazi zao hao, yaongezwe kwake (Kristo) ili aweze kuwapatia wanadamu wokovu kamili, kama baadhi ya watu wanaonekana kudhani; bali kwamba, bado kulikuwa na upungufu mwingi kwa upande wake kabla hajafananishwa kabisa na Mwokozi katika mateso yake.

Tafsiri ya kawaida ni, “yale yaliyosalia kwangu katika kustahimili dhiki kwa ajili ya Kristo.” Lakini hili linaonekana kuwa limepoa, na wala haliwezi kukidhi fikra za Mtume Paulo.

“Ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.” (Wafilipi 3:10-11)

Utukufu Una Yeye Milele na Milele; AMINA.

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *