Home 2021 December 24 Bethlehemu na Kalvari

Bethlehemu na Kalvari

Bethlehemu na Kalvari

“Jina tamu limeshuke toka mbinguni juu,

Ili kushinda upendo wa kina wa mioyo yetu, ili kutuvuta kwake;

Kama vile Bethlehemu na Kalvari inavyothibitisha!”

Tamko la Mtume Paulo kwamba “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi” (1 Timotheo 1:15) limeunganisha pamoja, yote mawili, Bethlehemu na Kalvari. Katika Bethlehemu Kristo Yesu alionyesha upendo wake kwa mwanadamu wote, sio kwa kuja tu na kuwa nasi, bali kwa kuwa mmoja wetu.

Luka, “tabibu mpendwa,” aliandika “Injili maarufu ya Luka Mtakatifu” ili kuonyesha jinsi Bwana Yesu Kristo alivyokuwa mwanadamu kikweli. Isipokuwa dhambi, Bwana wetu huyo alipata kuonja ‘mihemko’ yetu mingine yote – kama vile kuwa na huzuni, furaha, maumivu, n.k. Mwana wa Mungu kweli alifanyika Mwana wa Adamu ili wana wa wanadamu wapate kuwa wana wa Mungu.

Lakini maisha yake, peke yake, yasingeweza kutuokoa. Utakatifu wake ungefichua tu dhambi zetu na kutuhukumu. Hii ndiyo sababu Mtume Paulo anatangaza tena kwamba “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Wakorintho 15:3), na kwamba “TUNA UKOMBOZI KWA DAMU YAKE, MSAMAHA WA DHAMBI, KWA KADIRI YA UTAJIRI WA NEEMA YAKE” (Waefeso 1:7).

Wale wote wanaoamini hili na kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wao binafsi, leo wanafurahia ukweli wa shairi hilo hapo juu. Mioyo yao imevutwa kwa yule Mbarikiwa aliyetoka mbinguni hadi Bethlehemu na Kalvari kwa sababu YEYE aliwapenda UPEO…!!!

Utukufu Una Yeye Milele na Milele; Amina.

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *