Home 2021 December 08 Ombi Tusiloliomba Kamwe!

Ombi Tusiloliomba Kamwe!

Ombi Tusiloliomba Kamwe!

Kwa karne nyingi sasa, waamini wengi ‘wanyoofu’ wamekuwa wakiomba ombi hili: “Njoo, Bwana Yesu; njoo upesi,” lakini sisi tumeamua kutojiunga nao katika hili…

Ili tusije tukaeleweka vibaya, tunatanguliza maeleza kwamba hata sisi, tunatamani kumwona na kuwa pamoja na Bwana wetu aliyebarikiwa na kutukuzwa, na kama tukijifikiria sisi wenyewe tu; tungemtaka aje hata sasa – wakati huu, bila kukawia zaidi.

Lakini kuendelea kukawia huku kwa Bwana wetu, katika neema, ni somo maalumu la nyaraka za Mtume Paulo kama Mtume Petro asemavyo:

Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe” (2 Petro 3:15-16)

Je! Ni neema iliyoje kwa Bwana wetu kuchelewesha kurudi kwake kwa wale walio Wake na hukumu ambayo ingefuatia? Je! Ni neema kubwa kiasi gani kutuongezea siku ya neema mpaka sasa? Kwa kuwa sasa tumeokolewa, tungetamani kuwa pamoja na Yule tunayempenda na kumtamani, lakini Je! Ni kwa kiasi gani tunapaswa kumshukuru Bwana wetu kwa jinsi anavyotuvumilia na kuendelea kutungoja, na zaidi sana tunavyopaswa kuwa na hamu ya kuwavuta wengine Kwake huku Yeye akiendelea kutupa mda zaidi na zaidi?

Kwa kadiri tunavyotafakari juu ya wale ‘waliopotea’ na juu ya hatima yetu, kimsingi, hatutakiwi kumsihi Bwana “aje upesi,” ingawa kuja Kwake kwa ajili yetu kwa hakika ni “tumaini lenye baraka,” na tupo macho kuligonja litokee wakati wowote…

Katika muktadha huo, ni vyema ieleweke hapa kwamba sala, “Na uje, Bwana Yesu,” na ile inayofanana na hiyo – “Ee Mola, hata lini!” zote mbili ni sala za “wakati wa dhiki kuu”, zitakazotolewa na watakatifu (si wa Mwili wa Kristo) ambao wataishi wakati huo wa kutisha wa hasira ya Mungu. Sala zote mbili zinapatikana katika Kitabu cha Ufunuo na zote zinahusiana na kurudi kwa Bwana wetu duniani kuhukumu na kutawala, na sio kuhusiana na unyakuo wa Kanisa.

Katika Ufunuo 2:5 na 2:16 Bwana wetu anasema: “Basi tubu…; na usipotubu, naja kwako upesi,” yaani, kuhukumu. Katika Ufunuo 3:11 analiandikia kanisa la Filadelfia, lakini tena katika maonyo: “Tazama, naja upesi; shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Ufunuo 22:7 na 12 hutumiwa kwa maana hiyohiyo, ikionyesha kwamba katika siku hiyo ni wale tu “washindi” ambao watatamani sana Bwana aje na kukomesha uasi wa ulimwengu. Hivyo Yohana anafunga kitabu cha Ufunuo kwa tangazo hili:

“Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi”, na jibu lake ni: “Amina; na uje, Bwana Yesu” (Ufunuo 22:20)

Utukufu Una Yeye Milele na Milele; Amina.

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *