Home 2021 November 24 Wajibu wa Kila Mkristo!

Wajibu wa Kila Mkristo!

Wajibu wa Kila Mkristo!

Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima. Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi. Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia” (Warumi 1:14-16)

Mara tatu katika Warumi 1:14-16, Mtume Paulo ametumia kishazi “Nina”, na kila kishazi hicho kilipotumika, kimebeba ujumbe muhimu kwa kila mwamini wa kweli katika Kristo Yesu.

Anaanza katika Mstari wa 14 kwa kusema kuwa: “Nina deni – Nawiwa!” Mdeni kwa watu wote, kuwaambia kuhusu kazi ya wokovu ya Kristo Yesu. Lakini ni kwa nini hasa alikuwa na deni hilo kwa watu ambao hakuwahi hata kuwaona kwa sura? Kuna sababu kadhaa:-

Kwanza, mkononi mwake alikuwa na kile walichokihitaji watu wengine ili waokolewa kutoka kwenye adhabu na nguvu ya dhambi. Ukimwona mlevi amelala pembeni mwa njia ya reli na ukamwacha bila kufanya chochote kumsaidia mlevi huyo, na ikatokea amekanyagwa na kuuwawa na treni; Je! Wewe hutakuwa muuaji? Ikitokea nimemwona mtu anazama majini na mimi nina ‘boya la uhai’ mkononi mwangu lakini nisimtupie ndugu huyo kumsaidia; Je! mimi sitokuwa muuaji wa ndugu huyo ikitokea amezama? Tukiona mamilioni ya roho zilizopotea zimetuzunguka, huko tukijua ujumbe wa wokovu (Injili ya Neema), na tusiwaambie chochote ndugu ha; Je! Hatutakuwa na hatia kama watu hao watakufa bila Kristo?

Zaidi ya hayo, Paulo alijiona kuwa mwenye deni kwa wengine, kwa sababu Kristo ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zake pia alikuwa amekufa kwa ajili ya dhambi za wengine. Kama asemavyo katika 2 Wakorintho 5:14-15:

“Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao

Hatimaye, Kristo Yesu ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi za Paulo, alikuwa amemtuma aende kuwaambia wengine juu ya neema yake ya kuokoa. Ndivyo asemavyo katika 1 Wakorintho 9:16-17:

“Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili

Pili, Paulo anazungumzia hasa juu ya kile ambacho kila mwamini wa kweli anaweza kukisema: “Nina deni…; hivyo niko tayari kwa kadiri ya kile kilichomo ndani yangu” (Warumi 1:15). Alikuwa yuko tayari kulipa deni lake kwa sababu alikuwa na kile cha kulipia – “Habari njema ya neema ya Mungu.” Na kwa HAKIKA alifanikisha kuutangaza ujumbe huu kwa wengine, yeye binafsi pamoja na wale aliokuwa nao katika huduma.

Kwa mara ya mwisho, mara ya tatu; Paulo anatumia kishazi “Nina” kumaanisha kuwa: “Nina deni…; kwa hiyo niko tayari…; ndio maana siionei haya Injili ya Kristo, kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye…” (Mstari la 16). Paulo, wakati wote, alikuwa na fahari ‘kummiliki’ Kristo kama Mwokozi mkuu kutoka kwa dhambi.

Je! Wewe unamtambua Kristo hivyo; kwamba ni Mwokozi wako? Na Je! Unawaambia wengine kuhusu kazi yake timilifu wa UKOMBOZI pale Kalvari? Fanya hivyo, hilo ni JUKUMU LAKO BINAFSI…; ANZA SASA!

Utukufu na Ukuu na Uweza Vina Yeye Milele na Milele AMINA!

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *