Home 2021 October 15 Zawadi ya Bure Kwako!

Zawadi ya Bure Kwako!

Zawadi ya Bure Kwako!

Ni jambo lililo wazi  kwamba, siku hizi, kila kitu kinapanda gharama kwa haraka/kasi sana. Hakuna kinachoshuka bei; kila siku, bei za vitu vyote hupanda juu – zaidi na zaidi. Mishahara inapanda, ingawa sio kwa haraka/kasi kama gharama za maisha; kwani hata shilingi yetu, badala ya kupanga, inapungua thamani kila uchwao.

Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa sababu kuna jambo moja ambalo halijawahi kupanda bei – wokovu wa roho zetu za thamani. Haiko bei yoyote iliyowahi kuwekwa juu ya jambo hili na hayuko mtu atakayeweza kufanya hivyo kamwe, kwa sababu kadhaa muhimu:

  • Kwa sababu Mungu si masikini; Haitaji pesa zetu.
  • Kwa sababu ikiwa wokovu ungeweza kununuliwa, matajiri wangekuwa na faida/wangefaidika sana kuliko masikini.
  • Wokovu ulilipwa kikamilifu na Mungu Mwana juu ya msalaba wa Kalvari, na kwa hiyo kulipia senti hata moja ya ziada kwenye hilo ni sawa na kuinajisi kazi ya Msalaba ya Kristo.

Hata katika nyakati za Agano la Kale Mungu aliweka wazi kuwa dhabihu na kazi njema haziwezi kununua kibali chake. Katika Isaya 55:1-3, nabii alilia:

“Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara…”

Karne kadhaa baadaye, baada ya “injili ya neema ya Mungu” kukabidhiwa Paulo, Mungu alitoa vitu bora zaidi kwa wale ambao walikuwa tayari kuzipokea. Aliwatangazia waumini wa Kristo kwamba…

“wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (Warumi 3:24).

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7).

Wokovu umepewa bure, sio kwa sababu ni rahisi; HAPANA – BALI NI KWA SABABU HUWEZI KULIPA THAMANI YAKE!!!

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *