Home 2021 October 12 Imani Na Kusikia

Imani Na Kusikia

Imani Na Kusikia

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17)

Kifungu hiki muhimu cha Maandiko, tunasikitika kusema kuwa, hakijaeleweka miongoni mwa waamini. Watu wengi wanaifikiria imani kidhana tu, kana kwamba ina nguvu fulani ya kufikirika na kushangaza hivi.

Wanazungumza juu ya imani, lakini ni nini hasa wanachokimaanisha? Je, Ni imani katika nini? au Je, ni imani kwa nani? Hakika haiwezekani kuwa tu na imani, bila kuwa na ‘kitu’ au ‘mtu’ wa kuwa na imani hiyo.

Imani sio kuwa na bidii katika kutamani au kujiamini. Imani sio matumaini wala dhana wala fikra. Imani ni lazima iwe na msingi, iwe na nguzo! Kwa hivyo imani ya Mkristo imejengwa juu ya “Neno la Mungu” – juu ya kile ambacho Mungu amekisema katika Biblia.

Kifungu kilichotajwa hapo juu kinafafanua: “Imani chanzo chake ni kusikia.” Je, hilo sio jambo rahisi? Je, Halina ukweli wowote? Watu wengi wamesema kuwa “kuona ni kuamini,” lakini ukiwa unatafakari  vyema utagundua kwamba, msemo huu ni usemi wa kutokuamini.

Tukiwa tumeona jambo hatuhitaji kuamini tena; hilo limekuwa dhahiri kwetu. Lakini tunaposikia [au kusoma] jambo linaloripotiwa kwetu, tunaweza kuliamini au kulitilia shaka. “Imani chanzo chake ni kusikia.” Na vivyo hivyo kusikia huja kupitia kwa yale yaliyosemwa. Tunaamini, au tunakuwa na mashaka, juu ya kile tunachosikia na tunasikia kile kilichosemwa. Hivyo, imani ya Mkristo, huja kwa kusikia (kumsikia Mungu) na kusikia kwa Neno la Mungu. Imani yote ya kweli ya Kikristo imejengwa juu ya Neno la Mungu.

Kimsingi neno “kusikia,” katika Warumi 10:17, lina wazo la kutii – kusikia kwa lengo la kutii, kusikiliza kwa hamasa. Hii ndiyo sababu Wagalatia 3:5 inazungumza juu ya “kusikia kunakotokana na imani.” Na hivyo Waefeso 1:13, ikimmaanisha Kristo, inasema: “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu.” Kwa hiyo, tunasoma katika Yohana 5:24 pia, maneno haya ya Bwana Yesu:

“Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *