Home 2021 September 18 Enenda Zako Wala Usitende Dhambi Tena!

Enenda Zako Wala Usitende Dhambi Tena!

Enenda Zako Wala Usitende Dhambi Tena!

Waandishi na Mafarisayo, waliojihesabia haki, walikuwa wamemleta kwa Bwana Yesu mwanamke mmoja aliyefumaniwa katika uzinzi na “walipomweka katikati”, walianza kumshtaki, wakisema:

“Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?” (Yohana 8:4-5)

Ndugu hawa walikuwa wakimtumia mwanamke huyu aliyeanguka dhambini ili ‘kumlazimisha’ Bwana akubaliane nao kwamba mwanamke huyu anapaswa kupigwa mawe, au sivyo ‘ajibebeshe’ Mwenyewe shtaka la kukataa Sheria ya Musa.

Mwanzoni Yesu alijifanya “kana kwamba hakuwasikia”, lakini, walipoendelea kumshinikiza kwa kumuuliza, walikipata kile walichokuwa wakikitafuta! Akawajibu tu kifupi, kwa kuwaambia: “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe”; Bwana akainama chini, kufanya kile alichokuwa akifanya, ili kuiruhusu hukumu hiyo ifanye kazi yake ndani ya mioyo yao. Kabla, walikuwa “wamemweka katikati” yule mwanamke; Sasa Bwana alikuwa “amewaweka wao katikati” na, baada ya “kushtakiwa na dhamiri zao”, “wakatoka mmoja mmoja” (Mstari wa 9).

Na yule mwanamke alibaki amesimama “katikati” peke yake mbele yake Yesu: mwenye dhambi kubwa mbele ya Mwokozi Mkuu! Kwa kuwa hakuna hata mmoja wa Mafarisayo aliyethubutu kumtupia jiwe (yaani hakuna aliyemhukumu kuwa na hatia yule mwanamke), Bwana  – Mwokozi Mkuu, naye akasema: “Wala mimi sikuhukumu; Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (Mstari wa 11).

Ndiyo kusema, Bwana kwa neema, alimsamehe yule mwanamke mwenye dhambi, lakini bila kupuuza mahitaji ya Sheria. Bwana hakuwa amekataa kwamba yule mwanamke alistahili adhabu; Bali alikuwa ameonyesha tu kwamba Mafarisayo wenyewe nao walikuwa ni wenye dhambi; na ya kwamba wao pia, kama yule mwanamke, walihitaji Mwokozi.

Asante Mungu wetu! Kwa kuwa “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu”, Mungu anaweza kutusamehe – na atafanya hivyo, TUKIWA tu tunatambua dhambi zetu na hitaji letu la Mwokozi, na tusijiunge na kundi la wale wanaojiona kuwa ni watimilifu ambao wanaendelea kwenda “wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe” (Warumi 10:3).

“Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe WENYE DHAMBI…” (1 Timotheo 1:15). Mungu ni mwenye neema nyingi kwa wale ambao watakiri dhambi zao na hitaji lao la Mwokozi: “Kwa maana yeye yule ni Bwana wa wote, MWENYE UTAJIRI KWA WOTE WAMWITAO.”

“KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA” (WARUMI 10:12,13)

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *