Home 2021 July 25 Paulo na Kuzaliwa Upya

Paulo na Kuzaliwa Upya

Paulo na Kuzaliwa Upya

Ufunuo wa Paulo unatuongoza katika ukweli mtukufu wa kuheshimu vyote; msimamo wetu na uzoefu wetu, kama waamini. Ama hakika, kuzaliwa upya kwenyewe, kama inavyofanyika ndani ya mwamini leo, kunahusiana moja kwa moja na ubatizo wa kimungu ambao Kristo na mwamini wamefanywa kuwa wamoja.

Je! Kristo alifanywaje kuwa mmoja na wanadamu? Alibatizwa (aliingizwa) katika jamii ya wanadamu. Kristo hakuja tu kukaa na wanadamu, bali alikua mtu. Kivipi? Kwa kuzaliwa katika jamii ya wanadamu. Je! Hii ilikuwa kwa kuzaliwa kiasili? Hapana, bali kwa kuzaliwa kusiko kwa kiasili (supernatural). Alizaliwa kwa Roho Mtakatifu. Lakini ubatizo wake katika jamii ya wanadamu haukuishia tu kwa kuzaliwa kwake na maisha yake hapa duniani, bali alifanyika kabisa kuwa mmoja na wanadamu, hata alikufa kifo cha kibinadamu kwenye mti uliolaaniwa. Alibatizwa katika kifo (Luka 12:50) na, kama tunavyojua sasa, katika kifo chetu:

“Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe”

Na ni pale, pale Msalabani, ambapo tunakuwa kitu kimoja na Yeye. Wakati mtu ye yote yule anapoangalia tu Kalvari kwa imani, akikiri kwamba: “Yeye (Yesu) siye mwenye dhambi; Bali yeye ndiye mwenye dhambi. Na ya kwamba, Kristo anakufa kifo changu”; wakati huo huo anakuwa mmoja na Kristo; na kubatizwa katika Bwana aliyesulubiwa na aliyefufuka (Warumi 6:3; Wagalatia 3:26-27), katika Roho. Na kwa hiyo maisha mapya huzaliwa:

“Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?”

“Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo”

Kwa kuzaliwa kiasili? Hapana, kwa kuzaliwa kusiko kwa kiasili. Watu wengine (wafupi) ‘wanashikilia’ kwamba Nyaraka za Paulo hazifundishi juu ya kuzaliwa upya, jambo ambalo ni kosa. Mtume Paulo anafundisha ukweli huu juu ya kuzaliwa upya katika Tito 3:5, ambapo anasema:

“Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.”

Na katika 2 Wakorintho 5:17, Mtume Paulo anasema maneno haya juu ya mtu aliyezaliwa mara ya pili:

“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *