Home 2021 July 25 Kristo Mwana wa Mungu

Kristo Mwana wa Mungu

Kristo Mwana wa Mungu

Mtume Paulo anafungua Waraka wake kwa Warumi kwa kusema kwamba Bwana Yesu Kristo “alidhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu,” au “alitangazwa kwa nguvu kuwa Mwana wa Mungu… kwa ufufuko wake kutoka kwa wafu” (1:4).

Katika Zaburi 2:7, tunaye Kristo, katika unabii, akisema:

“Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”

Bwana wetu, kimsingi, alikuwa ni wa milele pamoja na Baba, lakini neno “nimekuzaa” hapa linatokana na sheria za Israeli, ikimaanisha wakati ambapo mtoto alitangazwa rasmi kuwa ni ‘mtu mzima’ (full-grown) na baba yake.

Lakini alikuwa hasa akimaanisha siku gani? Je! Ilikuwa ni siku gani hiyo, ambayo Baba (Mungu) alimtangaza Yesu rasmi kuwa:

“Leo nimekuzaa”?

Jibu linapatikana katika Matendo 13:33, ambapo Mtume anasema kwamba Mungu “alimfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.”

Kwa hivyo Bwana wetu alitangazwa rasmi na kwa nguvu, KUWA MWANA WA MUNGU, wakati wa kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Lakini ni nini hasa Mtume Paulo alichokimaanisha katika 2 Timotheo 2:7-8, aliposema maneno haya?

“Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama INENAVYO INJILI YANGU

Jibu ni kwamba wale kumi na wawili walikuwa wamemtangaza Kristo kama Mwana wa Daudi, ambaye atakaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi. Yao ilikuwa ni “injili ya ufalme.” Lakini wakati Mfalme na ufalme wake walipokataliwa, Mungu alimwinua mtume mwingine, Paulo, kutangaza “injili ya neema ya Mungu” (Matendo 20:24).

Kristo, hakika, alifufuliwa kutoka kwa wafu ili aje kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi, na hili bado litakuja kutokea, lakini Mtume Paulo ana ujumbe mwingine kwetu, wakati huu wa sasa: kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu ili kudhibitisha haki yetu na kuwa Mkuu wa “Kanisa ambalo ni Mwili Wake.”

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *