Home 2021 June 30 Acha Kutafuta Mapenzi ya Mungu

Acha Kutafuta Mapenzi ya Mungu

Acha Kutafuta Mapenzi ya Mungu

Kabla ya kujifunza kuyatambua mapenzi ya Mungu kupitia kugawa kwa usahihi Neno la Mungu, ni kawaida kuwa katika safari ndefu ya maisha ya kiroho bila kuyajua au kugundua mapenzi ya Mungu.

Bila kuwa na mgawanyo ulio sahihi, Biblia hugeuka kuwa ‘msitu mnene’ ambao anayetembea humo hawezi kuona mwanga na hivyo kushindwa kuelewa ujumbe wake, na kwa sababu hivyo, tunabaki kuangalia matamanio ya mioyo yetu na hali za maisha yetu kuwa ndio ‘dalili’ ya mapenzi ya Mungu.

Tunabaki kujiambia tu kuwa matukio ‘yasiyojulikana’ yapo mikononi mwa Mungu, na hivyo tunachukua hatua zenye upofu kuelekea hatima ya malengo ya maisha yetu huku tukibaki kuwa wajinga wa mapenzi yake.

Huu wote ni ukengeufu, na kubwa zaidi lipo: tunafanya mapenzi yetu wenyewe, na kwa ubatili, tunayaita ya Mungu…

Ni uwongo kusema kwamba mapenzi ya Mungu hayafahamiki. Na ni uongo mkubwa zaidi kusema kwamba tunaweza kufanya mapenzi ya Mungu bila kuyajua mapenzi Yake hayo kuwa ni nini!

Ikiwa huyajui mapenzi ya Mungu, basi huwezi kufanya mapenzi ya Mungu. Ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza uyajue.

Ikiwa huyajui mapenzi ya Mungu, kamwe huwezi kuishi maisha katika Kristo. Kutoyajua mapenzi ya Mungu, kunatuhukumu kifo…

Ikiwa huyajui mapenzi ya Mungu, na unaendelea kusema unaishi maisha yako kwa ajili ya Bwana, unajidanganya mwenyewe. Ukweli ni kwamba, unafanya mapenzi yako mwenyewe, huku ukiyaita kuwa ni mapenzi ya Mungu. Huo ni uasi…!!!

Kuligawa neno la kweli ya Mungu kwa usahihi ni ‘mshale’ mkubwa na wa ‘kipekee’ unaokuelekeza kwenye mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi katika Biblia.

Jifunze mapenzi ya Mungu hapa: 1 Timotheo 2:4, Waefeso 1:9-10, Waefeso 3:8-10, na 1 Wathesalonike 5:16-18.

“Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana” (Waefeso 5:15-17).

Itakuwa ni busara kwako kuacha kuyatafuta, kwa maana yanajulikana!

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *