Home 2021 May 16 Yesu Hakuwahi Kukosea Popote!

Yesu Hakuwahi Kukosea Popote!

Yesu Hakuwahi Kukosea Popote!

Kama unajikuta unashikilia imani ambayo inadhani kuwa kuna kitu chochote ambacho Yesu aliwahi kukisema kilikuwa na makosa, jitafakari sana na ujiulize nani ni mwalimu wa uwongo!

Hapa chini kuna orodha ya baadhi ya sehemu maarufu ambazo “Wakristo” waliodanganywa wanadhani Yesu alikosea:

  • “… Yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke” (Mathayo 19:4)
  • “… Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri” (Mathayo 19:17)
  • “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele …” (Mathayo 25:46)
  • “… Kwa maana huyu [Paulo] ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli” (Matendo 9:15)

Yesu aliwajua Adamu na Hawa.

Yesu alifundisha sheria kwa ajili ya uzima kwa Israeli.

Yesu alifundisha juu ya hukumu ya milele na kuzimu.

Yesu alibadilisha kila kitu alipomtuma Paulo kuhubiri neema yake!

Je! Inawezekana kuwa Yesu amekosea? Nafasi hiyo HAIPO!

Je! Unaweza kuwa wewe umekosea? Mara kwa mara…

Chochote utakachojifunza kutoka kwenye maandiko (Biblia) ni lazima kianze na kuishia kuwa Yesu ni MKWELI. Ili kudumisha kiwango hiki, kunahitajika kugawa neno la kweli ya Mungu sawasawa.

Kwa Utukufu Wake Yesu Kristo

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *