Home 2021 May 16 Ayubu Alichokililia Sisi Tunacho

Ayubu Alichokililia Sisi Tunacho

Ayubu Alichokililia Sisi Tunacho

Ukristo wa kisasa unamtaka Mungu azungumze nao…!

Wanataka Mungu awaambie kwa nini mambo fulani yanatokea, awaambie kusudi Lake kwao, na awaambie pia mapenzi Yake kwao.

Hiki ndicho kilikuwa kilio cha Ayubu kwa Mungu. Ayubu aliteseka, hakujua kwanini, na hivyo alimlilia Mungu amjibu.

Ukristo wa kisasa unamwiga Ayubu na kulia kilio chake. “Wakisema, Bwana! Umenibwaga topeni, Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. Nakulilia wewe, wala huniitikii; Nasimama, nawe wanitazama tu” (Ayubu 30:19-20).

Ayubu alikuwa ni mjinga kifundisho. Ndivyo ilivyo kwa Ukristo wa kisasa, lakini angalau Ayubu alikuwa na sababu za msingi…!

Ayubu aliishi kabla ya Biblia kuandikwa. Katika upweke wake na kukata tamaa alisema:

“Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!” (Ayubu 31:35)

Kile Ayubu alichokuwa anakitaka ni kitabu. Baadaye, Mungu alikiandika.

Biblia inatuambia juu ya mapenzi ya Mungu, kusudi lake, na kwa nini mambo mabaya yanatokea, na juu ya wokovu.

Ayubu alikuwa na kisingizio cha kulilia, hakuwa na Biblia ya kupatia maarifa juu ya kusudi la Mungu. Alisema, kama angekuwa nayo:

“Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifungia mfano wa kilemba” (Ayubu 31:36)

Wakristo wanaodhani kuwa wako kama Ayubu leo ​​ni ‘wapumbavu’. Ayubu hakuwa na Biblia, na wala yeye au marafiki zake wote hawakuielewa siri ya Kristo (Ayubu 15:8):

Tunayo Biblia na tunaweza kusoma. Siri imefunuliwa! Udhuru wetu ni nini?

Nakuhimiza, kithamini kitabu hicho cha Mungu …

Uweza na Ukuu Una Yeye Milele Yote

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *