Home 2021 May 13 Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi

Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi

Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi

Moja ya nyaraka zenye kuelimisha zaidi katika Biblia, na kwa hakika iliyosheheni maarifa juu ya wokovu zaidi ya vitabu vingine vyote, ni Waraka muhimu sana wa Mtakatifu Paulo kwa Warumi.

Paulo, kwa asili na kwa mafundisho, alikuwa ni mtu wa mantiki na labda ni mwenye kujenga hoja kimantiki mkubwa zaidi wa wakati wote, na katika jambo hili maneno yake yaliongozwa na Roho wa Bwana, ili kwamba katika Waraka wake huu kwa Warumi tuwe na hoja yenye nguvu juu ya Mungu na mwanadamu, kulaaniwa na kuhesabiwa haki. Ni jambo jema na la kushangaza sana kuona mpango wa Mungu wa wokovu kwetu ukielezwa kwa uwazi hivyo na Mtume huyu. Jambo hili linakosekana sana katika uinjilisti wetu wa kisasa.

Hoja yenye mantiki ya fundisho katika waraka huu wa Warumi imeanza na kuonyesha upotovu wa maadili ya wanadamu WOTE. Inasema, hata kwa wale wanaojiona kuwa ni waadilifu (wanaojihesabia haki):

“Mtu uwaye yote, huna udhuru…” (2:1)

Mtume huyu kisha anaendelea kuonyesha kwamba Sheria ilitolewa, sio kwa kusudi la kumsaidia wanadamu kuwa mwema, bali “ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu” (3:19). Hitimisho lake ni kuwa:

“Hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (3:20)

Mtume Paulo anasisitiza hoja yake zaidi kwa kuonyesha jinsi Bwana Yesu Kristo alivyojitoa mwenyewe kama malipo tosha kwa dhambi zetu ili tuweze “kuhesabiwa haki bure kwa neema [ya Mungu], kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (3:24). Hitimisho lake tena ni:

“Twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria” (3:28)

“Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (5:1)

Hatimaye Paulo anaonyesha jinsi wale wanaomtumainia Kristo “walivyobatizwa katika Kristo” (6:3), na jinsi walivyofanywa wamoja pamoja naye kwa imani. Hitimisho lake la mwisho ni kuwa:

“Hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (8:1)

Na Mtume huyu, aliyejaliwa hekima ya kipekee na Mungu (2 Petro 3:15), anafunga sehemu ya fundisho la waraka huu mkuu kwa kusema:

“Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?” (8:31-35)

Ushauri wetu kwa wale mwenye maswali juu ya wokovu:

WASOME kwa KUTAFAKARI Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi, kwa kutumia akili zao wenyewe na kwa maombi!

Utukufu una YEYE, Milele na Milele, AMINA.

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *