Home 2021 May 10 Uamsho wa Kweli

Uamsho wa Kweli

Uamsho wa Kweli

Katika siku za nabii Ezra, Israeli ilikuwa katika hali sawa na ya Kanisa leo. Cha kufurahisha, hata hivyo, viongozi wengine wa wakati huo walihukumiwa mioyoni mwao kwamba walikuwa wakipuuza Neno la Mungu – haswa ile sehemu ambayo ilikuwa imeelekezwa kwao: sheria ya Musa.

Kwa sababu hiyo, wakaamua kumjengea Ezra mimbari ambayo angeweza kusimama na kuwasomea watu maandiko (Nehemia 8:4). “Kuanzia asubuhi hadi saa sita mchana” aliwasomea maandiko hayo, wakati wengine walijichanganya na wasikilizaji na “kuwasababisha watu kuelewa.”

“Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa. Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa” (Mstari wa 8, 12)

Vivyo hivyo, baada ya Bwana wetu, Yesu Kristo, kuwafunulia (kuwafafanulia) Maandiko wale wanafunzi wawili njiani kwenda kijiji cha Emau, waliambiana wenyewe kwa wenyewe:

“Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?” (Luka 24:32)

Vikundi vingi vyenye nia nzuri na watu binafsi kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiomba bure kwa ajili ya uamsho wa kweli wa kiroho katika Kanisa, lakini njia pekee ya uhakika ya uamsho ni kuwa na nia mpya ya kuijua Biblia, na hasa kwa kile Mungu anachokisema kwetu kupitia nyaraka za Mtume Paulo.

Tunapohukumiwa katika mioyo yetu kwa kupuuza kwetu Neno la Mungu kama linavyopatikana katika Nyaraka za Mtume Paulo; wakati watu wa Mungu “wanapojifunza” ili “kuligawa” Neno na kuanza kulifundisha kutoka kwenye mimbari, uamsho mkubwa wa kiroho bila shaka utafuata lakini, ole ipo kwa sababu watu wengi wa Mungu wameridhika sana; wameridhika sana na taaluma duni ya kuingia kwenye uzoefu huu uliobarikiwa.

Kinyume na hayo, pale tutakapojifunza Neno la Mungu sisi wenyewe, na haswa sehemu ile ya Neno Lake ambalo limelengwa hasa kwetu; sisi, kama ilivyokuwa kwa Waisraeli wa siku za Ezra, tutapata raha ya kuelewa barua ya upendo wa Mungu iliyoandikwa kwetu.

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *