Home 2021 May 08 Sababu 21 Kwa Nini Uache Kutoa Zaka

Sababu 21 Kwa Nini Uache Kutoa Zaka

Sababu 21 Kwa Nini Uache Kutoa Zaka

Katikati ya watumishi wa Mungu leo, kuna matumizi mabaya ya maandiko ambapo fundisho la ‘zaka’ linatumika kutoa kwenye sheria ya Musa ili kulirudisha kanisa nyuma na kuliweka chini ya laana. Jambo hili linapaswa kukomeshwa (Tito 1:11). Yesu Kristo alilifundisha kanisa la kipindi cha Paulo njia bora zaidi ya kutoa bila sheria.

Hapa chini kuna orodha ya sababu kadhaa ambazo zitakuonyesha ni kwa nini unapaswa kuacha kutoa zaka:

  1. Hatupo chini ya sheria ya kutoa zaka

Zaka ilikuwa ni sehemu ya sheria. Sisi Kanisa, Mwili wa Kristo, hatupo chini ya sheria hiyo. (Warumi 6:14)

  1. Sheria ya kutoa zaka ni dhaifu

Zaka inayotakiwa kutolewa haiwezi kubadilisha moyo au nia. (Mathayo 23:23, Wagalatia 4:9, Warumi 8:3)

  1. Sheria ya kutoa zaka ni duni

Kutoa fungu la kumi siku zote uhitaji kutoa zaidi. Hii sio zawadi, bali ni kutimiza wajibu wa sheria (Wagalatia 4:9).

  1. Kanisa sio watu wa agano la Mungu

Maagano yote mawili, lile la zamani na jipya, yalifanywa na Israeli na Yuda na kwa hiyo mahitaji yake hayakuwahi kuwalenga kwa watu wa mataifa (Waebrania 8:8) Mataifa wangeweza kubarikiwa kwa kuliheshimu na kuibariki Israeli, na kuabudu Mungu wa Israeli.

  1. Hakuna ukuhani wa Kilawi leo

Zaka maarufu leo ​​ni ile zaka iliyokwenda kwa ukuhani wa Walawi (Hesabu 18:21):

“Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania”

 Hakuna ukuhani wa Walawi leo!

  1. Nafasi ya Mchungaji sio ya kikuhani

Wahubiri, Wachungaji, Waalimu, n.k., katika Kanisa Mwili wa Kristo leo sio ‘Makuhani’. Yesu Kristo ndiye mpatanishi pekee, kati ya Mungu na Mwanadamu (1 Tim 2:5).

  1. Haturithi ardhi ya Israeli

Zaka iliyotolewa kwa Walawi ni kwa sababu hawakuwa na urithi wa ardhi ya Israeli (Hesabu 18:21).

  1. Hakuna dhabihu za hekaluni tena

Kwa kuwa Kristo alilipa yote kwa damu yake, hakuna haja tena ya kulipa (zaka) ili mtu mwingine afanye huduma hiyo.

  1. Kanisa la mahali pamoja si mbadala wa hekalu

Je! Hamjui kwamba ninyi ni hekalu la Mungu? (1 Wakorintho 3:16)

  1. Kanisa halifuati sherehe za siku za sikukuu zinazohitajika

Ilikuwa ni mara tatu kwa mwaka katika Kumb. 16:16. Katika siku fulani za sikukuu, katika mahali patakapochaguliwa, ndipo zaka zilitolewa. Kuna zaka ‘moja’ ilikuruhusu ukae nyumbani na kuitumia (kuila wewe mwenyewe) kwa kile unachotaka (Kumb. 14:26):

“Na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako”

  1. Mahitaji ya kutoa zaka yalikuwa ni zaidi ya asilimia 10

Kumb. 14:28 ni mfano mmoja wa zaka juu ya ongezeko kila baada ya miaka 3 ambayo ilikuwa juu ya zaka ya kawaida ya Walawi.

  1. Baraka za kimwili hazitolewi tena

Sheria ya zaka ilifundisha baraka za kimwili kwa Israeli kutoka kwa Mungu kwa sababu ya zaka zao (Malaki 3:10). Bila kuwa na agano na Mungu – ukuhani, ahadi, au kutoa zaka ya hekalu ili upate faida – vyote havitafanya kazi na ni kujilisha upepo.

  1. Kristo amelipa kanisa baraka zote za rohoni

Baraka hizo ziko katika ulimwengu wa roho katika Kristo (Waefeso 1:3)

  1. Mungu anatupa mahitaji yetu yote bila kutoa zaka

Umewahi kuisoma Wafilipi 4:19? Inasema hivi:

“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”

Kwamba Mungu atakupa mahitaji yako kulingana na uwingi utajiri wake katika utukufu katika Kristo, na sio kwa sababu ‘ume-zaka’! Je, unaweza kuyaamini maandiko?

  1. Kutoa fungu la kumi kunakulazimisha kushika sheria yote

Angalia Wagalatia 5:3, Yakobo 2:10

  1. Amani na Mungu hupatikana bila kutoa zaka – Warumi 5:1

“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo”

  1. Tunatakiwa kufanya kazi kwa ajili ya mahitaji yetu katika kipindi hiki cha neema ya Mungu

Mtume Paulo ameweka wazi kuwa mtu asiyefanya kazi na asile (2 Wathesalonike 3:10). Yaliyopo kwenye Mathayo 6:11 na Malaki 3:10 hayafanyi kazi leo. Paulo amezidi kutuonya katika 1 Timotheo 5:8 kuwa kama tutashindwa kuwatunza walio wa nyumbani mwetu, sisi tu wabaya zaidi kuliko hata wale wasioamini na ya kwamba TUMEIKANA IMANI.

  1. Zaka ilitakiwa, ilikuwa ni lazima

Kutoa leo sio “kwa lazima” bali ni kwa “ukarimu” (2 Wakorintho 9:7). Hii ndiyo tofauti muhimu kati ya ukarimu na wajibu.

  1. Sheria ya zaka inakuweka chini ya laana

“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye” (Wagalatia 3:10)

  1. Kristo amekukomboa kutoka kwenye sheria ya zaka

Kuendelea kutoa fungu la kumi ni kuthibitisha ukosefu wa maarifa ya nini Yesu alikikamilisha msalabani na kupuuza kazi hiyo ya msalaba wa Yesu Kristo. Zingatia haya:

“Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure” (Wagalatia 2:21)

“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti” (Wagalatia 3:13)

“Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika” (1 Wakorintho 1:17)

  1. Aya zinazohusu ‘zaka’ katika Biblia

Mwanzo 14:17-20                   Amosi 4:2-6

Mwanzo 28:20-22                 2 Nyakati 31:1-12

Walawi 27:30-34                   Nehemiah 10:37-38, 12:44, 13

Hesabu 18:19-28                   Malaki 3:7-10

Kumb. la Torati 12:1-19       Mathayo 23:23

Kumb. la Torati 14:22-29   Luka 11:42

Kumb. la Torati 26:12-13    Luka 18:9-14

1 Samweli 8:14-17                 Waebrania 7:1-19

 

Katika aya zote hizi, zaka wakati wote ilikuwa ni chakula tu, kutoka nchi takatifu ya Mungu!

Zaka haikutokana na fedha

Hoja moja inayotolewa na ‘wala zaka’ ya kuunga mkono utoaji wa zaka ‘isiyo ya chakula’ ni kwamba fedha haikuwepo kipindi kile ndio maana alitaka zaka za chakula/mazao! Hoja hii sio ya kibiblia na ni ushahidi mwingine kuwa watu hao hawazisomi Biblia zao na kuzielewa.

Katika kitabu cha Mwanzo peke yake, “fedha” imetokea katika maandishi, mara 32 na neno hilo linatokea mara 44 kabla ya zaka kutajwa kwa mara ya kwanza katika Mambo ya Walawi 27. Neno shekeli pia linaonekana mara nyingi kutoka Mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati:

“Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu” (Mwanzo 13:2).

“Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako” (Mwanzo 17:12)

“Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako. Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara” (Mwanzo 23:15)

NB:

Maarifa haya hayakusudii kuzuia kutoa kwa ukarimu kwa sababu za Bwana. Mungu anapenda ukarimu kama kielelezo cha shukrani zako kwake. Wakati maarifa haya yanaelezea ni kwa nini fundisho la Paulo linakufundisha kuacha kutoa zaka, Mungu hafundishi ukarimu haba!

“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu” (2 Wakorintho 9:7)

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

7 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *