Home 2021 May 01 Toka Imani Hata Imani

Toka Imani Hata Imani

Toka Imani Hata Imani

“Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani” (Warumi 1:16-17)

Sababu ambayo ilimfanya Paulo asiwe na ‘haya’ (asione aibu) juu ya injili ya wokovu ni kwa sababu injili ndiyo inaifunua haki ya Mungu. Hiyo ni, injili ya “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Wakorintho 15:1-4) inayofunua jinsi Mungu asivyozifuta dhambi zetu kwa kuzifunika chini ya sakafu na kutuficha kwa kutupitisha mlango wa nyuma wa mbingu wakati shetani akiwa amefumba macho yake (au amesinzia) – hatuangalia! Mungu anaweza kutuokoa kwa ‘haki’ kwa sababu Mwanawe alikufa ili kulipa deni la dhambi zetu.

Hivyo, tunapoamini injili ya wokovu, Mungu humwokoa kwa uaminifu wake “kila atakayeliitia jina la Bwana” (Warumi 10:13). Ikiwa unajiuliza ni kwanini inampasa kusema hivyo, na kwanini anaweza kushawishiwa kufanya vinginevyo, ni kwa sababu ya aina ya watu ambao wakati mwingine humwita! Wewe na mimi tunaweza kuwa na mawazo mengine juu ya kuwaokoa watu kama (wa aina ya) Sauli wa Tarso, wauaji wa kawaida ambao waliamini injili kabla ya kufa kwao. Lakini Mungu huwaokoa wote kwa uaminifu wake, wale wanaoiweka imani yao katika Kristo.

Na hivyo ndivyo injili ilivyo nguvu ya Mungu iletayo wokovu “toka imani hadi imani.” Neno “imani” linaweza kumaanisha uaminifu, kama ilivyo katika Warumi 3:3. Hivyo Warumi 1:17 inasema kwamba wokovu unatiririka/unamiminika kutoka kwenye uaminifu wa Mungu wa kumwokoa mtu yeyote kwenda kwa yeyote anayemwamini Kristo – kutoka imani ‘yake’ hadi imani ‘yetu’. Hivi ndivyo ambavyo “nafsi ya mtu… isiyo na unyofu” au isiyo haki (Habakuki 2:4) inaweza kufanywa kuwa yenye haki (2 Wakorintho 5:21), na kisha “mwenye haki ataishi” (awe na uzima wa milele) – “kwa imani yake.”

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *