Home 2021 April 20 Yaliyotabiriwa Vs Yaliyoshuhudiwa

Yaliyotabiriwa Vs Yaliyoshuhudiwa

Yaliyotabiriwa Vs Yaliyoshuhudiwa

Kama ilikuwa ni Paulo ndiye ‘aliyefunua’ kwamba Kristo alijitoa mwenyewe kuwa fidia (ukombozi) “kwa ajili ya wote” (1 Timotheo 2:6) kinyume na kuwa fidia ya “wengi” katika Israeli (Mathayo 20:28), tunaielezeaje Yohana 1:29?

“… Yohana amwona Yesu … akasema, Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”

Yohana alikuwa nabii (Luka 7:28), na manabii hawakuelewa unabii wao wenyewe kila wakati (1 Petro 1:11-12), haswa wakati pale unabii wao huo unapohusiana na “mateso ya Kristo.” Mungu alijua bila shaka kwamba hii ingewasumbua manabii, ndio maana aliwafariji kwa kuwaelezea kwamba “hiyo haikuwa ni kwa ajili yao wao wenyewe, bali ni kwa ajili yetu sisi wao walihudumu katika mambo hayo” ambayo wao waliyatabiri.

Tunajua kwamba hakuna mtu, kati ya wale waliomsikia Yohana akitoa kauli yake hiyo, alielewa kuwa Kristo atakufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu; kwa sababu hata wale Thenashara 12 walimsikia Yesu mwenyewe akinena yayo hayo, nao hawakuelewa (Luka 18:31-34). Hata Shetani naye hakuelewa (1 Wakorintho 2:7-8), kama angeelewa, ‘asingemchochea’ Yuda Iskariote amsaliti Bwana Yesu (Luka 22:3-4).

Kwa hiyo ‘fidia’ ambayo Kristo Yesu aliifanya kwa wanadamu wote ilikuwa imetabiriwa katika Yohana 1:29, lakini haikuwa imeshuhudiwa mpaka pale “wakati uliofaa” ulipokuwa umewadia kwa Paulo “kuwekwa wakfu kuwa mhubiri na mtume” (1 Timotheo 2:6-7):

“Ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli”

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *