Home 2021 April 19 Ukweli Usiopingika

Ukweli Usiopingika

Ukweli Usiopingika

Mkanganyiko wa kitheolojia katika Kanisa leo hii, kimsingi ni matokeo ya uasi wake dhidi ya mamlaka ya Paulo kama mtume aliyeteuliwa na Mungu kwa kipindi cha sasa cha neema ya Mungu:

“Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini” (Waefeso 3:1-12)

Takribani kutoka kila upande, Paulo anatajwa tu kama mmoja wa mitume, wakati mwingine hata kama mmoja wa wale Thenashara kumi na wawili, ingawa kumbukumbu ya Maandiko inathibitisha kwamba hangeweza kufuzu kuwa mmoja kati ya hao kumi na wawili (Angalia Mathayo 19:28 na Matendo ya Mitume 9:1).

Katika Wagalatia 1 na 2 Mtume Paulo anatupa ‘cheti’ cha utume wake, kana ilivyokuwa kwa wale waliomhoji wakati wa siku zake. Paulo, anafungua hoja yake kwa kutoa tamko:

“Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo” (Wagalatia 1:11-12)

Maandiko yanatufundisha pasina shaka yoyote kwamba utume wa Paulo na ujumbe wake ulikuwa wa kipekee kabisa na tofauti na ule wa wale kumi na wawili au wa yeyote yule mwingine aliyemtangulia. Hivi ndivyo Jumuiya ya Kikristo, kwa ujumla wake, imekataa kukubali ukweli huu. Je! Hii ni ajabu? Ndiyo maana wanachanganya mpango wa Mungu wa ufalme uliotabiriwa na mpango wa Mungu wa “siri,” uliowekwa kwa Paulo kwa ajili yetu Kanisa katika kipindi hiki cha sasa!

Maandiko yanasisitiza sio tu matumizi ya mara kwa mara ya Mtume ya kiwakilishi cha mtu wa kwanza – “mimi”, “yangu”; lakini pia tabia ya kipekee ya utume na ujumbe wake.

Puuza ukweli huu, kuchanganyikiwa ni lazima; kuukubali ukweli huu, mapingano mia kadhaa yanayoonekana katika maandiko hutoweka!

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *