Home 2021 April 12 Sheria Ilivyoeleweka Vibaya!

Sheria Ilivyoeleweka Vibaya!

Sheria Ilivyoeleweka Vibaya!

Kuna maoni matatu potofu ambayo watu wengi wanayo juu ya Sheria ya Mungu na Amri zake zile Kumi:

  1. Watu wengi wana maoni yasiyo sahihi kwamba sheria hizo zilikuwapo siku zote (tangu kuumbwa kwa ulimwengu) na kwamba alipewa mwanadamu wa kwanza, yaani Adam, au pengine kipindi kifupi baadaye. Ukweli ni kwamba, Mungu alimpa Musa sheria hizo kwa ajili ya Israeli takribani miaka 1500 kabla ya Kristo; hii inakadiriwa ni kama baada ya miaka 2500 ya historia ya wanadamu kupita (Yohana 1:17). Kwa hivyo wanadamu waliishi duniani kwa karibu miaka 2500 bila Sheria au Amri Kumi za Mungu!
  2. Watu wengi hufikiria kwamba Sheria na Amri Kumi zilitolewa kwa wanadamu WOTE kwa jumla; lakini ukweli ni kwamba, Sheria na Amri hizo walipewa Israeli peke yake (Kumbukumbu la Torati 5:1-3): “Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda. Bwana, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai”
  1. Watu wengi hufikiria kwamba Sheria na Amri Kumi zilitolewa kutusaidia kutenda haki. Hata ‘watumishi’ wengi wa Mungu hufundisha hivyo, ingawa Biblia yenyewe inatufundisha wazi kabisa kwamba Sheria na Amri hizo zilitolewa ili kutuonyesha kuwa sisi ni wenye dhambi.

Ni kweli kwamba sheria, wakati ilipotolewa kwa Israeli, pia ilikuwa inamwonyesha mtu wa Mataifa kwamba yeye naye ni mwenye dhambi. Hii ndiyo sababu Warumi 3:19 inasema hivi:

“Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu

Lakini jambo la muhimu zaidi kupita yote ni kuwa: Ni watu wachache sana wanatambua kwamba Bwana Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili kutukomboa kutoka kwenye hukumu ya HAKI ya sheria. Hii inafundishwa vyema sana na Mtume Paulo katika Maandiko yafuatayo:

“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Wagalatia 3:13-14)

“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21)

“Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema” (Warumi 6:14)

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *