Home 2021 April 12 Kumtambua Kristo Ipasavyo!

Kumtambua Kristo Ipasavyo!

Kumtambua Kristo Ipasavyo!

Yohana Mbatizaji alimtambulisha Bwana wetu, Yesu Kristo, kwa tangazo hili:

“Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 3:2)

Katika huduma yake yote ya kidunia Kristo alijulikana kama “Mwana wa Daudi”, mfalme ambaye Mungu alifanya agano naye kuanzisha Ufalme Wake wa milele.

Manabii wa Agano la Kale walitabiri kwamba Kristo, na Yeye atatawala duniani, juu ya kiti cha enzi cha baba yake Daudi. Wakati Ufalme Wake ulipokuwa ukitangazwa kuwa “umekaribia”, yeye Yesu alikuwa akitembea na kuzungumza na kula na watu kama “Mwana wa Mtu (Adamu)”. Akiwa amechoka kutokana na urefu wa safari, Yesu aliketi kwenye kisima cha Yakobo na kuomba maji ya kunywa. Akikabiliwa na umati mkubwa wa watu, aliingia kwenye mashua ya uvuvi na kuhutubia umati huo kutoka baharini. Alichukiwa na wapinzani wake, alijaribiwa, akapigwa mijeledi, akatemewa mate, na kupigiliwa misumari kwenye mti. Kwa kweli huyu alikuwa “Kristo aliyejidhihirisha katika mwili”!

Kuhusiana na aibu yake, hata hivyo, Mtume Paulo anasema, kwa uvuvio wa kimungu kwamba: “Mungu alimwadhimisha (alimtukuza) mno, na akamkirimia (kumpatia) Jina lililo juu ya kila jina (yaani lipitalo majina yote)” (Wafilipi 2:9).

Tena, Mtume huyo pia anatangaza kwamba nguvu kuu ya uweza wa Mungu “ilitenda ndani ya Kristo, alipomfufua kutoka kwa wafu, na kumkalisha mkono wake wa kuume katika nafasi za mbinguni, MBALI SANA, ZAIDI YA VYOTE …” (Waefeso 1:19-21).

Hajulikani tena kama “Yesu wa hali ya chini”, BALI kama “BWANA” aliyeinuliwa juu sana huko mbinguni. Na hii inatuhusu sisi pia:

” Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena ” (2 Wakorintho 5:16)

Mwokozi wetu Yesu sasa anajulikana kama Mwana wa Mungu aliyetukuzwa, Mgawaji/Mtoaji Mkuu wa Neema kwa mwanadamu aliyepotea; Yeye ambaye kwa upendo na huruma yake “alionja mauti kwa ajili ya kila mtu” (Waebrania 2:9).

Kwa Utukufu wa Jina Lake

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *