Home 2020 October 07 Ulimwengu Bila Baba

Ulimwengu Bila Baba

Ulimwengu Bila Baba

Biblia inasema kina baba wana jukumu la kuzaa watoto wanaotembea kwa kumstahili Mungu (1 Wathesalonike 2: 11-12):

“Vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia; ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.”

Watafiti wa kijamii wamegundua mara kwa mara kuwa watoto wasio na baba wana uwezekano mkubwa wa…

  • Kufa utotoni
  • Kuishi katika umasikini
  • Kujiua
  • Kuteseka na unene kupita kiasi
  • Kuacha shule
  • Kutumia dawa za kulevya na pombe
  • Kukabiliana na unyanyasaji na utelekezwaji wa watoto
  • Kuingia katika ushoga
  • Kupata ujauzito katika ujana
  • Kubakwa au kutoa mimba
  • Kuacha Kanisa na kukataa mila za kiroho
  • Kushiriki katika magenge ya kihalifu na mauaji
  • Kufanya uhalifu na kuishia gerezani

Suluhisho lenye athari zaidi kwa shida zilizo hapo juu za kijamii sio kwenye ‘nyumba za serikali’, bali ni nyumbani. Kina baba wanaweza kuubadilisha ulimwengu kwa kubadilisha mfumo wa maisha katika nyumba zao.

Kina baba wanaoishi nyumbani huwa wako “hai” katika maisha ya watoto wao kuliko wale ambao huwa hawaishi nyumbani.

Ikiwa ukosefu wa wababa ni shida kubwa, basi hiyo inamaanisha kuwa Mungu alikuwa yuko sawa wakati wote kwa kuwapa kina baba jukumu la kulea watoto katika malezi na maonyo ya Bwana (Waefeso 6:4):

“Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”

Bila baba ulimwengu ungekuwa mahali pabaya zaidi!

Mungu na ashukuriwe kwa ajili ya baba

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *