Home 2020 October 05 Ukristo Unaanza na Ufufuko

Ukristo Unaanza na Ufufuko

Ukristo Unaanza na Ufufuko

Ukristo unafundisha ufufuo wa watu wote ili waweze kumkabili Muumba wao katika hukumu.

Bila Kristo watu wote watahukumiwa, lakini wakiwa na Kristo watu wote wanaweza kuishi katika haki ya milele, amani, na furaha.

Hii inawezekana tu kwa sababu Kristo alichukua hukumu yetu juu yake yeye mwenyewe, kwa njia ya msalaba, na anatoa haki yake bure kwa wote wamwaminio.

Ikiwa Kristo hakufufuka, hangeweza kutoa “ofa” yoyote kwetu.

Hili ni tumaini. Hii ni hakika. Hakika hili, linategemea ufufuko!

Je! Tunawezaje kujua tumeokolewa?

Sio kwa matunda yetu. Sio kwa sababu ya kujitolea kwetu. Sio kwa sababu tuna imani. Ni kwa sababu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu…

Huu ni ujumbe ambao utashudia roho zikiokolewa.

Uinjilishaji sahihi na kuishi kwa neema lazima kujumuishe ufufuko, kuanzia na kufufuka kwa Kristo.

Kwa Utukufu Wake

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *