Home 2020 September 24 Tuheshimu Tofauti – Yenye Tofauti; Yametofautiana!

Tuheshimu Tofauti – Yenye Tofauti; Yametofautiana!

Tuheshimu Tofauti – Yenye Tofauti; Yametofautiana!

Ufunguo wa kuelezea mgawanyiko sahihi ni kwa watu kuona tofauti zilizopo katika Biblia Takatifu.

Kwa mfano, ukweli wa SIRI wa ‘mwili mmoja’ ni kwamba hakuna tofauti iliyopo kati ya Myahudi na Myunani katika Kristo Yesu (Wagalatia 3:28; 1 ​​Wakorintho 12:13).

Ushirika wa SIRI hii haufanyi tofauti yoyote kati ya Myahudi na Mmataifa. Hata hivyo, SIRI hii haina maana yoyote mpaka tofauti kati ya Myahudi na Mmataifa katika siku za nyuma iheshimiwe na kuwekwa wazi.

Katika jitihada za kujaribu kumwonyesha mtu tofauti hiyo ni rahisi kumwambia, “kitabu hiki kiliandikwa kwa Israeli”, au “hiyo ilikuwa kwa Wayahudi na sio watu wa Mataifa”, lakini taarifa hizi zinakuwa hazina maana (zinagonga mwamba) kwa mtu ambaye haelewi tofauti hiyo.

Watu hao wanadhani hakuna tofauti leo kwa sababu hawajui tofauti iliyokuwepo wakati uliopita. Hii ndiyo sababu inayowafanya wanachukua kila agizo lililopo kwenye Biblia na kulifanya kuwa lao. Inaweza isiwe ni kushindwa kuigawa kweli ya neno la Mungu sawasawa; bali ni kwa sababu hawakujua kama kuna hiyo tofauti ya kuigawa.

Tunahitaji kuwasaidia kuona ukweli huu kwa kuwaelezea kwamba kulikuwa na tofauti kubwa ambayo ilikuwepo hapo awali kati ya Israeli na Mataifa. Myahudi na Mataifa walikuwa tofauti sana: Mungu alitoa upendeleo maalum na ahadi kwa taifa la Israeli pekee na sio kwa watu wa Mataifa.

Msikie jinsi Paulo anavyoifanya hiyo kazi kwetu: “…kumbukeni ya kwamba ninyi, mlio watu wa Mataifa… zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio na maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani” (Waefeso 2:11-12).

Ni mpaka hapo tu watakapo heshimu kile Mungu alichokifanya tofauti katika wakati uliopita ndipo tu watakapoweza kuona kwa uwazi kwa nini umoja wa ushirika tulio nao leo ni tofauti. Ni tofauti na kile Mungu alichokuwa akikifanya hapo awali.

Huu ni mwanzo wa mgawanyiko sahihi (2 Timotheo 2:15).

Alivyovitenganisha Mungu, mwanadamu na asiviunganishe!

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *