Home 2020 September 06 Nidhamu ya Kiroho

Nidhamu ya Kiroho

Nidhamu ya Kiroho

Kuna njia mbili za kuishi na kufanya uchaguzi/maamuzi katika maisha yako. Ambazo ni:

  1. Kulingana na kile unachojua.
  2. Kulingana na kile unachohisi.

Unapofanya maamuzi ya kufanya kazi kulingana na kile unachojua, bila shaka utafaulu katika maisha yako. Unajua unahitaji kufanya kazi ili upate uwezo wa kumudu mahitaji mbalimbali. Kuna wakati unajisikia kama uache vile, lakini unakuwa huna namna, kwani unajua una jukumu la kuitunza familia yako na usipoitunza utajisikia kama umekosa kuwajibika hivi.

Wakati kile unachokijua na kile unachokihisi vinatofautiana, nidhamu huwa inahitajika. Nidhamu hapa huwa ni kutengeneza tabia ya kuishi kulingana na kile unachojua, kinachotofautiana na kile unachohisi.

Hii haina tofauti na maisha yako katika Kristo. Roho na mwili huwa vinapingana (Wagalatia 5:17). Roho inakuambia kile unachokijua kuhusu wewe kuwa ni nani katika Kristo, na mwili wako nao unakusukuma juu ya kile unachokihisi. Nidhamu ya kiroho inahitajika hapa ili uweze kuishi kulingana na kile unachojua, kinyume cha kile unachohisi.

Nidhamu ya kiroho sio ibada inayokuleta karibu na Mungu, au kitendo cha kujitolea ambacho kinakupa hisia za kiroho. Nidhamu ya kiroho inafanya kazi kulingana na kile unachokijua juu ya Kristo aliyeko ndani yako.

Unajua utu wako wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo (Warumi 6:6). Ingawa unahisi ushawishi wake kila siku. Hapa inabidi utambue kuwa utu wako huo wa kale umekufa kulingana na kile unachokijua.

Unajua kwamba hauko chini ya sheria. Ingawa unahisi “laana” yake wakati wote unaposhindwa kufikia viwango vyake vitakatifu (Warumi 7:24).

Unajua kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yako (1 Wakorinto 3:16), ingawa humsikii/huhisi uwepo wake.

Unajua mapenzi ya Mungu yalivyo, kulingana na maandiko matakatifu yaliyogawanywa sawa (1 Timotheo 2: 4; 1 Wathesalonike 4: 3; 1 Wathesalonike 5:18), ingawa hauhisi Roho ikikuongoza. Roho ni Mungu. Unapaswa kufanya kazi kutoka kwenye kile unachojua katika Mungu.

Unapofanya uamuzi wa kufanyia kazi kulingana na kile unachojua, ni hakika utafaulu katika maisha yako. Hii lakini, inahitaji Nidhamu!

Kama kile unachokijua ni ‘Kristo ndani yako’, ni hakika kwamba utafanikiwa katika maisha haya ya sasa na hata yale yajayo (1 Timotheo 4:7-8). Hii inahitaji nidhamu ya kiroho ili kuishi katika ujuzi na ufahamu wa kiroho uliopatikana kutoka kwa neno la Mungu lililogawanywa sawasawa (Wakolosai 1: 9).

Nidhamu ya kiroho sio kitendo unachokifanya, bali ni kutengeneza tabia ya kuishi kulingana na kile unachokijua.

Ongeza/Kuza ufahamu wako juu ya nafasi uliyonayo (wewe ni nani) katika Kristo na jinsi ya kutembea katika Roho kwa kujisomea zaidi, wewe mwenye binafsi katika Warumi 6-8.

Kwa Utukufu wa Jina Lake

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *