Home 2020 August 30 Maombi Pasina Majibu?

Maombi Pasina Majibu?

Maombi Pasina Majibu?

Watu wanapofika sehemu ya kuona kuwa Mungu anaweza asijibu maombi yao wanayompelekea, mara nyingi hufikiria kwamba maombi yao yamekuwa ya bure na yasiyo na maana.

Wanafikiri kuwa, “ikiwa siwezi kupata kile nilichoomba, maombi sasa yanakuwa na maana gani?”

Ikiwa hili ndilo tatizo lako, basi ujue kuwa tatizo halipo katika maombi ambayo unadhani kuwa hayana matunda, bali tatizo lipo juu ya jinsi wewe unavyowaza juu ya utendaji kazi wa maombi hayo.

Maombi sio sanduku la kukusanyia maoni la Mungu au njia ya kuweka hitaji lako kwa maongozo ya Mungu. Kusudi la maombi sio kumfanya Mungu atimize matakwa yako au mahitaji yako yote.

Fikiria ikiwa hivi ndivyo jinsi ulivyokuwa ukifanya kila wakati ulipokuwa na mawasiliano na familia yako au marafiki zako!

“Ikiwa siwezi kupata kitu chochote kutoka kwako, basi kuna haja gani ya mimi kuzungumza na wewe, au kufikiria jambo lolote juu yako, au kuwa na mahusiano na wewe, au kuwa marafiki?”

Je! Huo sio aina ya ubinafsi? (Jibu sahihi ni, NDIO.)

Bila shaka, kusudi la Mungu ni kukufanya wewe ukue kiroho, na maombi ni mwenendo wa kiroho ambao unamwimarisha na kumtia nguvu mtu wako wa ndani sawasawa na yalivyo mapenzi ya Mungu, na sio yako.

Maombi sio kitu cha bure, hata kama mahitaji yako ya kimwili hayakukidhiwa, kwa sababu maombi yanapaswa kuelekeza moyo wako na akili zako kwa Kristo (Wafilipi 4:7).

Hilo ndo lifanyikalo, kila wakati uombapo!

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *