Home 2020 August 24 Kutafuta Ishara

Kutafuta Ishara

Kutafuta Ishara

Hapo mwanzo Mungu aliumba jua, mwezi, na nyota kuwa ishara na nyakati na misimu (Mwanzo 1:14). Hii inaelezea usahihi wa kihesabu wa kuwepo kwao na ukadiriaje wetu wa kisayansi wa kutokea kwao.

Lakini ‘wasukuma’ unabii wanakwenda mbali zaidi na kuzipita zamani za kalenda na kusema wao ndiyo ishara za nyakati za mwisho za unabii wa Kibiblia.

Mungu, kwa hakika, aliwaambia Israeli juu ya ishara maalum zitakazotokea angani ambazo zingeandamana na utimilifu wa unabii fulani (Yoeli 2:31).

Hata Paulo anasema…

“Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima” (1 Wakorinto 1:22)

Hii ndio sababu hasa, kwa nini Mwili wa Kristo hauitaji ishara, na wala haujaambiwa uzitafute!

Mwili wa Kristo Hauitaji Ishara

Katika mwili wa Kristo, hakuna Myahudi wala Myunani (Wakolosai 3:11; Wagalatia 3:28). Sisi sio Wayahudi; kwa hiyo hatuitaji ishara!

Kila kitu tunachohitaji kujua kwa ajili ya utendaji wetu kama kanisa kimefunuliwa katika ufunuo wa SIRI ya Kristo, na sio kupitia ishara katika nyota, jua au mwezi.

Wokovu wetu sio kitu ambacho kitakuja katika nyakati za mwisho, bali ni kitu ambacho tayari kimeshafika! Kiko hapa Katikati yetu sasa (Warumi 5:11; 2 Wakorinto 6:2)!

“Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa” (Tito 2:11)

Tunatakiwa kuweka fikira zetu juu ya vitu vilivyo juu zaidi kuzipita nyota, na hatupaswi kuweka fikira zetu katika vitu vilivyo chini, katika nchi (Wakolosai 3: 2).

Israeli iliambiwa itafute ishara katika mbingu ili iweze kujua ni lini Kristo atarudi na kukaa nao. Lakini kulingana na mpango wa SIRI, Kristo yuko ndani yetu tayari (Wakolosai 1:27).

Nyakati za mwisho za unabii wa Biblia (na ishara inazoambatana nazo) hazitaanza tena kwa Israeli hadi hapo Mungu atakapomaliza huduma yake ya upatanisho kupitia mwili wa Kristo.

Nguvu za Mungu Aliye Juu

Mungu ndiye mwenye nguvu zote za kutengeneza nyota na ishara zingine zozote zile katika anga; lakini hata hivyo, sio nyota au ishara ambazo zinadhihirisha nguvu ya Mungu leo: bali ni Kristo (Warumi 1:16). Wokovu leo haupo kwenye ishara, bali upo katika Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

Badala ya kuzihitaji ishara, Paulo anasema hivi:

“bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu” (1 Wakorinto 1:23-34)

Kutokuona (kukosa) ishara ni kikwazo kwa wale waliokwama kwenye unabii. Kuhubiriwa kwake Kristo ni upuzi kwa wasomi na wanasayansi ambao wanayatafuta majibu ya dhambi kisayansi.

Ishara pekee tuliyonayo katika wokovu ni msalaba ulio tupu na kaburi lililo wazi la Mwokozi wetu Yesu Kristo (Wagalatia 6:14). Hiyo ndiyo ishara ambayo ulimwengu wote unahitaji kujua habari zake, na tumeamriwa kuhubiri habari zake.

Nitainua macho yangu kutazama mambo ya kushangaza yaliyo katika mbingu yaliyoanza tangu wakati wa uumbaji wa Mungu, lakini sitatafuta ishara kutoka kwa Mungu wakati Bwana Yesu Kristo ameniagiza niwaangazie watu wote wajue habari za madaraka na ushirika wao wa ile SIRI (Waefeso 3:9). Jukumu letu ni kuwafanya watu wote waelekeze mawazo yao katika hekima ya kweli na nguvu ya Mungu ambayo ipo katika INJILI ya Kristo Yesu, na sio katika kutafuta ishara.

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *