Home 2020 August 20 Kanisa Kabla ya Paulo

Kanisa Kabla ya Paulo

Kanisa Kabla ya Paulo

Watu wanaposikia wazo la kugawa nyakati sawa sawa na kwamba fundisho kwa ajili ya Kanisa la leo kuwa linapatikana katika nyaraka za Paulo pekee, swali lisilo epukika wakati wote huwa ni hili:

Mbona Kulikuwepo na Kanisa kabla ya Paulo?

Hakika lilikuwepo!

Tafakari kutajwa kwa Kanisa hilo kabla ya kuokolewa kwa Paulo:

“Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa” (Matendo 2:47b)

Bwana naye alikuwa ameshatoa maelekezo kuhusu Kanisa lake katika Mathayo 16:18 na Mathayo 18:17.

Paulo mwenyewe anasema kabla ya kuokolewa kwake “alilitesa Kanisa la Mungu”, jambo ambalo limethibitishwa na Luka katika Matendo 8:3:

“Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani” (Matendo 8: 3)

Kama huo sio ushahidi wa kutosha juu ya uwepo kwa kanisa kabla ya Paulo, yapo pia mahubiri yaliyovuviwa na Roho Mtakatifu ya Stefano kwenye Matendo 7 ambapo analitaja kanisa lililokuwepo kabla ya Kristo!

“Huyu ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai” (Matendo 7:38a)

Ndio kusema, kulikuwa na kanisa jangwani ambalo lilipokea sheria ya Mungu huko Mlima Sinai!

Neno ‘kanisa’ halipatikani mahali popote katika agano la kale, isipokuwa neno linalofanana na hilo, lenye asili ya Kiebrania, linalotafsiriwa ‘kusanyiko la walioitwa’ na ambalo linapatikana mara mamia kadhaa likimaanisha kusanyiko la wana wa Israeli, na kama vile ilivyonenwa na Stefano pia katika Matendo 7:38.

Ni wazi kwamba kanisa, au kusanyiko la Mungu, linapatikana katika maandiko yote, lakini kwa hakika kanisa la leo ni tofauti na kusanyiko la Mungu, Musa aliloliongoza jangwani. Lakini ni kivipi?

Kuhama kutoka kwenye Ujumla kwenda kwenye Upekee

Neno ‘kanisa/kusanyiko’ kwenye Biblia ni neno la jumla, kama vile watoto. Tunaweza kusema baba ana watoto kadhaa, na itakuwa ni kweli pia kuwa tukimwona mmoja wa watoto hao, tutajua kuwa ni mmoja wa watoto wa yule baba.

Lakini hata hivyo, kwa kufanya hivyo, hatutatambua tofauti iliyokuwepo kati ya watoto hao. Hatutajua, kwa mfano, ni yupi kati ya watoto hao tunamtafuta bila ya kupata maelezo ya ziada.

Mtoto mmoja anaweza kuwa ni mvulana, mwingine msichana. Mtoto mwingine anaweza kuwa amepewa jukumu la ‘kiuongozi’ la kuwasimamia watoto wengine, wakati mwingine anaweza kuwa amepewa jukumu la kufagia nyumba, na mwingine kuosha vyombo.

Ni dhahiri kwamba kutakuwa na mtoto mkubwa, na mtoto mdogo zaidi. Kulikuwepo na wakati ambapo mtoto mdogo hakuwapo, lakini baba huyo bado alikuwa na watoto. Kuna wakati sasa ambapo mtoto huyo mdogo amezaliwa, na baba sasa ana mtoto mwingine mpya (mdogo).

Tunaweza kukutana na neno ‘kanisa’ au ‘kusanyiko’ katika maandishi yote, na hiyo itakuwa ni sawa na kusema kwamba baba amekuwa na watoto wakati wote. Hata hivyo, ikiwa tunataka kujua majukumu yetu ya kipekee na utambulisho wetu, ni lazima tuheshimu ukweli kwamba kama vile baba anavyoweza kuwa na watoto tofauti, ndivyo pia kulivyo na makanisa (makusanyiko) tofauti katika maandiko.

Je! Kanisa ni nini?

Imesemwa mara kwa mara kwamba kanisa ni kusanyiko la walioitwa, eklesia, au kusanyiko la watu wa Mungu. Maana hiyo, hata hivyo, inashindwa kutambua mabadiliko katika asili, utendaji, na ujumbe wa watu hao wa Mungu katika maandiko yote.

Asili ya “kanisa jangwani” ilikuwa ile ya taifa kutoka kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Asili ya kanisa leo sio ile ya taifa, bali ni kiumbe kipya kinachoitwa mwili wa Kristo, mwili wa kiroho uliotengenezwa (ulioundwa) na watu kutoka mataifa yote.

Utendakazi wa “kanisa jangwani” ulikuwa ni kulingana na maagano ambayo Mungu alikuwa amewapa watu hao. Utendaji wa kanisa leo ni kulingana na ushirika wa siri ya Kristo.

Ujumbe wa “kanisa jangwani” ulikuwa ule wa sheria, haki na ufalme wa Mungu duniani. Ujumbe wa kanisa leo ni ule wa injili ya neema ya Mungu, haki ya bure kwa imani, na kuketishwa pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu.

Wakati Wote Lilikuwepo Lakini Tofauti

Ni wazi kwamba kanisa limekuwepo wakati wote katika maandiko yote. Kwa uwazi huo huo, inapaswa kufahamika kwamba kumekuwapo na makanisa tofauti pia kulingana na asili yao, utendaji, na ujumbe. Hili limekuwa wazo la kugawa nyakati sawa sawa, wakati wote!

Kanisa jangwani sio kanisa la leo, mwili wa Kristo. Vivyo hivyo, kanisa huko Yerusalemu (Matendo 8: 1) ambalo lilikuwa wakati wa Pentekoste lilikuwa na asili, utendaji, na ujumbe tofauti kuliko kanisa la leo.

Kama tutalielezea kanisa kwa kutokuangalia tu maana yake ya jumla kama “kusanyiko la watu wa Mungu”; bali kwa asili yake, utendaji wake, na kwa ujumbe wake, basi hatutaliona kanisa hilo la leo katika Mathayo 16, Matendo 2, au Matendo 7, isipokuwa katika nyaraka za Paulo ambazo kipekee zinaelezea siri ya kanisa, Mwili ‘mmoja’ wa Kristo.

Je, kulikuwa na kanisa kabla ya Paulo? NDIYO! Je, lilikuwa na asili sawa, utendaji unaofanana, na ujumbe sawa kama wa kanisa linaloelezwa na mtume Paulo? HAPANA!

Je, vitu vyote vitajumlishwa pamoja katika Kristo katika utimilifu wa nyakati? Ndio (Waefeso 1:10). Ni kweli, kulikuwa na kanisa kabla ya Paulo, lakini lilikuwa TOFAUTI!

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *