Home 2020 March 09 Je, Musa Aliikana Torati Yake?

Je, Musa Aliikana Torati Yake?

Je, Musa Aliikana Torati Yake?

Ni kwanini unadhani, Musa aliyatamka maneno haya, mwisho wa huduma yake? Na je, ni kwanini Mtume Petro naye aliyarudia maneno hayo ya Musa? Vipi, kuhusu Stefano naye, ni kwa nini aliyarejea maneno hayo ya Musa, wakati anakabiliana na Wayahudi waliomwua kwa mawe?

Kama Roho wa Mungu, ameruhusa maneno haya ya Musa, yaandikwe (tena mara tatu) kwenye Biblia, unadhani hayana UMUHIMU wowote? TAFAKARI…

Kumbukumbu la Torati 18:15

“Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye”

Matendo ya Mitume 3:22

“Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi”

Matendo ya Mitume 7:37

“Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye”

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *