Home 2020 March 05 Je, Mathayo, Marko, Luka, na Yohana ni Vitabu wa Agano la Kale?

Je, Mathayo, Marko, Luka, na Yohana ni Vitabu wa Agano la Kale?

Je, Mathayo, Marko, Luka, na Yohana ni Vitabu wa Agano la Kale?

Kila mwanafunzi wa kawaida wa Biblia anajua kwamba sehemu ya Agano Jipya la Biblia huanza na vitabu vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Pia tunaweza kujua kwamba asili ya mgawanyo huu inatokana na lugha tofauti ambazo kutoka kwazo vitabu hivyo vimetafsiriwa.

Hata hivyo, kutaja sehemu ya Kiyunani ya maandiko kama Agano Jipya inaweza ikawa ndio uwezekano wa asili ya matatizo mengi watu waliyonayo katika kuelewa huduma ya Yesu duniani. Kwa mujibu wa maandiko, wingi wa ‘taarifa’ hizi nne juu ya maisha ya Bwana wetu Yesu Kristo, HAKIKA ni Agano la Kale.

Waebrania 9:15-17 inasema hivi:

“Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya”

Waebrania 9:15-17 inaeleza kwamba ilikuwa ni baada ya kifo cha Yesu, ndipo Agano Jipya lililipopata nguvu. Wagalatia 4:4 inaelezea zaidi kwamba:

“Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria

Sheria ya Musa ilikuwa ndio utaratibu wa Agano la kale. Kulingana na Wagalatia 4:4, Yesu alizaliwa na kuishi chini ya Agano la Kale. Ilikuwa ni mpaka baada ya kifo chake ndipo Agano Jipya ndipo lingeweza kupatikana. Kwa kuwa sehemu kubwa ya taarifa ya vitabu hivyo na huduma nzima ya Yesu duniani ilitokea kabla ya kifo chake, basi ni lazima ichukuliwa kwamba vitabu hivi vinne bado viko katika muktadha wa Agano la Kale.

Hii inaelezea kwa nini Paulo aliandika kwamba Yesu alikuwa mhudumu kwa watu waliotahiriwa ili kuzithibitisha ahadi zilizofanywa kwa mababa:

“Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu” (Warumi 15:8)

Hii pia inaweza kuelezea kwa nini Yesu alihudumu kulingana na Agano la kale:

Alitahiriwa (Luka 2:27)

Alibatizwa kwa maji (Mathayo 3:15)

Alifundisha msamaha wenye masharti (Mathayo 6:14)

Alifundisha utoaji wa sadaka ya kilawi kwa ajili ya uponyaji (Mathayo 8:4)

Alifundisha kuzishika amri (Marko 10:17-19)

Alifundisha kuwatii Mafarisayo (Mathayo 23:2-3)

Alishikiri sikukuu za Kiyahudi (Mathayo 26:17)

Ili kuelewa vyema maandiko, tunahitaji kuelewa muktadha wa vifungu tunavyosoma. Kwa hiyo, ni muhimu kutambua kwamba matukio yaliyotangulia au yaliyotokea kabla ya msalaba katika Mathayo, Marko, Luka na Yohana yako ndani ya Agano la Kale.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *