Home 2020 March 02 Ubatizo Katika Biblia

Ubatizo Katika Biblia

Ubatizo Katika Biblia

Ni kosa la kawaida kufikiri kwamba ubatizo wa maji (mengi au machache) ni bora zaidi wakati huu kuliko ubatizo mwingine katika Biblia. Hata hivyo, Biblia inataja ubatizo wa aina nyingi na ubatizo wetu ‘mmoja’ haujumuishi maji. Hapa chini, kuna orodha ya ubatizo wa aina mbalimbali katika Biblia, ikiwa ni pamoja na ule mmoja ambao upo katika utendaji leo, kama ilivyofundishwa na Bwana wetu Yesu Kristo kulingana na ufunuo wa ile siri.

“Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Waefeso 4:5)

Ubatizo mmoja ambao utendaji kazi leo ni ubatizo wetu katika (ndani ya) Kristo kwa Roho. Huu ndio ubatizo pekee uliofundishwa na Mtume wetu Paulo (1 Wakorinto 12:13; Warumi 6:3; Wagalatia 3:27; Wakolosai 2:12).

Aina mbalimbali za ubatizo zinazoelezwa katika Biblia ni hizi zifuatazo:

Ubatizo wa aina ya Nuhu

Mtume Petro anataja kwamba watu wanane waliokolewa kwa maji katika safina kama aina ya ubatizo wa baadaye (Mwanzo 6:13; 1 Petro 3:20-21).

Ubatizo kwa Musa (wawe wa Musa)

Paulo anawasilisha (anauelezea) ubatizo wa Israeli kwa Musa “katika wingu” na “baharini” (1 Wakorinto 10:1-2; Kutoka 14:29).

Sherehe za Utakaso za Israeli

Tamaduni hizi za utakaso zilihitajika chini ya sheria ya Musa kwa utakaso wa watu (Hesabu 19:13; Walawi 11:25; Kutoka 19:14; 30:17-21; Waebrania 9:10).

Ubatizo wa Ukuhani wa Lawi

Miosho ya namna hii ilihitajika ili kuwa kuhani chini ya sheria ya Musa (Kutoka 29:4; Mambo ya Walawi 8:6; Hesabu 8:7).

Ubatizo wa Kijadi wa Kiyahudi

Ubatizo huu hauwakuwa na mamlaka chini ya sheria ya Musa lakini ulikuwa ni sehemu ya mila ya Kiyahudi (Mathayo 15:1-2; Marko 7:1-9; Luka 11:38).

Ubatizo wa Yohana

Yohana alikuja kwa Israeli akibatiza kwa maji kwa ajili ya ondoleo la dhambi ili waweze kuingia katika ufalme uliohaidiwa (Mathayo 3:5-6; Marko 1:4; Luka 3:3; Yohana 1:31; Luka 7:29; Matendo ya Mitume 10:37).

Ubatizo wa Yesu (Aliobatizwa na Yohana)

Yesu, ambaye hakujua dhambi, alibatizwa na Yohana ili kutimiza haki yote (Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-10).

Ubatizo wa Moto

Yesu angelibatiza taifa la Israeli kwa moto wakati taifa hilo lingekuwa linapita katika dhiki kuu. Ubatizo huo wa kupita katika majaribu ungewatupa watu wasio waaminifu kuzimu (Isaya 4:4; Malaki 3:2-3; Mathayo 3:11; Luka 3:16).

Ubatizo wa Yesu katika Kifo

Ubatizo wa pili wa Yesu ambao aliutimiza pale msalaba ambapo alibebeshwa/alizamishwa kwenye dhambi za Israeli na za ulimwengu (Mathayo 20:22; Marko 10:38; Luka 12:50).

Ubatizo wa Maji wakati wa Pentekoste

Wakilisho la Petro la ubatizo wa maji kwa ajili ya ondoleo la dhambi katika jina la Yesu (Matendo 2:38; Marko 16:16; Mathayo 28:19; Matendo 22:16; Ezekiel 36:25).

Ubatizo wa Roho wakati wa Pentekoste

Huu ni ubatizo wa Roho Mtakatifu uliofanywa na Yesu Kristo kutoka mbinguni uliomwagwa juu ya sazo (remnant) la waumini wa Israeli kwa ishara na nguvu zikiwafuata (Isaya 44:3; Mathayo 3:11; Marko 1:8; Luka 24:49; Matendo 2:17-18; Matendo 8:15-17; Matendo 11:16).

Ubatizo wa Mataifa wa Kornelio

Kornelio alibatizwa na Roho Mtakatifu kama ishara kwa Petro. Petro, hatimaye, akawabatiza Kornelio na wanataifa wengine, waliokwisha kujazwa na Roho Mtakatifu tayari, kwa maji (Matendo 10:45-48).

Ubatizo kwa Ajili ya Wafu

Ubatizo huu umejadiliwa na kushindaniwa sana na zaidi upo uwezekano wa kufanana au kuwa ni jina mbadala la moja ya batizo zingine. Kama hii ni kweli, “kwa ajili ya wafu” ingeonyesha hali ambayo wale waaminio walibatizwa (1 Wakorinto 15:29).

Ubatizo katika Kristo

Ubatizo pekee uliofundishwa na Paulo ambao humtambulisha muumini pamoja na Kristo, katika kifo chake, kuzikwa kwake na katika ufufuko wake pia. Ubatizo huu hufanywa na Roho na hauna (haujumuishi) maji (1 Wakorinto 12:13; Waefeso 4:5; Wakolosai 2:12; Wagalatia 3:27; Warumi 6:3-4).

UTUKUFU UNA YEYE KRISTO MILELE NA MILELE AMINA.

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *