Home 2020 February 13 Kazi ya Maombi

Kazi ya Maombi

Kazi ya Maombi

Maombi hufanya kazi ya kuzalisha amani ya Mungu ambayo utunza maisha yetu kikamilifu (Wafilipi 4:6)

Maombi hufanya kazi ya kuzifanya haja zetu zijulikane na Mungu (Wafilipi 4:6)

Maombi hufanya kazi ya kuhifadhi mioyo yetu na nia zetu  kwa Amani ya Mungu ipitayo akili zote (Wafilipi 4:7)

Maombi hufanya kazi ya kututia hamasa ya kuhudumu kama vile ambavyo Bwana ametuagiza. (Waefeso 6:19)

Maombi hufanya kazi ya kuteka mateka mawazo yote (Wafilipi 4:8, 2 Wakorinto 10:5)

Maombi hufanya kazi ya kutupatia nguvu za kiroho na ujasiri (Waefeso 3:12-16)

Maombi hufanya kazi ya kuzalisha shukrani kwa Mungu (1 Wathesalonike 5:17-18)

Maombi hufanya kazi ya kutufanya tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa na ustahivu (1 Timotheo 2:2)

Maombi hufanya kazi katika kuidhihirisha neema ya Mungu katika maisha yetu

Maombi Hufanya kazi!

Maisha yangu ya kiroho yangekuwa yamekufa kama pasingekuwa na neno la Mungu na maombi.

Omba kwa shukrani, omba kwa furaha, waombee na wengine, omba bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17).

Kwa Utukufu wa Jina Lake

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *