Home 2020 February 11 Sura Mbili za Yesu

Sura Mbili za Yesu

Sura Mbili za Yesu

Hizi ni sura mbili za Yesu – Yesu ambaye hajafa na Yesu ambaye amekufa! Ni lazima ujue kuwa, ni mmoja tu kati ya hao wawili ndiye anayeokoa kwa sasa, katika majira ya haya ya uachilio wa NEEMA YA MUNGU! Hiyo peke yake inakupasa kuwa makini juu ya yupi katika hao wawili unatakiwa umhubiri!

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16)

Katika mistari yote hiyo miwili, Yohana na Paulo, wote wanazungumzia upendo wa Mungu wa kuokoa watu wake. Lakini Yohana anamzungumzia kuaminiwa kwa Yesu katika mwili, Yesu ambaye alikuwa katikati ya walio wake, ili awaokoe! Kinyume na Yohana, Paulo anamzungumzia Yesu aliyekufa ili azibebe dhambi zetu sisi tuliokuwa hatuna mamna ya kujikomboa wenyewe, anazungumzia kazi ya Msalaba kuwaokoa waovu!

“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8)

Wakristo karibu wote, wamehubiriwa Yohana 3:16, hivyo kuwafanya wakose kujua kuna mstari ‘dada’ wa hiyo Yohana 3:16 ambao unabadilisha kabisa maana ya wokovu – namna ambayo Mungu sasa anawaokoa watu wake; sio kwa kuamini ‘utoto pekee wa Yesu’ BALI kwa kuamini kuwa Kristo alikufa, alizikwa na alifufuka kwa ajili ya wokovu wetu (1 Wakorinto 15:1-4)

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *