Home 2020 February 10 Msamaha wa Dhambi

Msamaha wa Dhambi

Msamaha wa Dhambi

MSAMAHA WA DHAMBI

Je, Ni Nani Awezaye Kuupokea Msamaha wa Dhambi Toka kwa Mungu?

Kujibu swali hilo, ni vyema tuanze kwa kusoma Kitabu cha Matendo 13:38-39 ambacho kinasema hivi, “Basi na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi; na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.”

Msamaha ni nini na kwanini tunauhitaji?

Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo na kulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, kuachilia au kufutilia mbali kosa au deni. Tunapomkosea mtu, tunaomba msamaha kwao ili turudishe uhusiano uliokuwepo kabla. Msamaha hautolewi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa, la hasha, kwani hakuna mtu anayestahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwingine, haijalishi amekukosea kiasi gani.

Biblia inatuambia kwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 inasema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika hukumu na adhabu ya milele tukitesekaa kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46; Yohana 3:36).

Namna ya kuupokea Msamaha

Msamaha unatakiwa upokelewe Kwa shukrani, Mungu ni mwenye upendo na huruma kwetu, ni mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu zote! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo ni jukumu letu kuupokea msamaha wetu kutoka kwa kwake kwa moyo wa shukrani, ni neema yake tu ndiyo imetuokoa.

Adhabu na haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo tuliyositahiri kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu – Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa msalabani kwa kuichukua adhabu ya kifo ambayo kwanza tulistahili sisi, yaani mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanywa kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akiichukua adhabu tuliyo stahili! Mungu, kwa kifo chake Yesu, alitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 inasema hivi, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, una hisia za kuudhi na za mara kwa mara, na zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu kuepukika? Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia mbali deni lile tukapate kusamehewa na kuhesabiwa haki. Unacho takiwa kufanya ni kumwomba Mungu akusamehe dhambi zako kupitia kwake Yesu Kristo, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha wa dhambi, naye atatusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii njema sana, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”

Je, ni jambo rahisi kusamehe dhambi?

Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza tu  kuupokea, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo peke yake ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Sala kama hii hapa chini, ni njia moja wapo ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupa msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chake na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaungama na kuziacha dhambi zangu zote na nina weka imani yangu na tumaini langu kwako ili niokolewe.

Asante kwa neema yako kuu na ya ajabu kwangu na kwa msamaha, Amina.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *