Home 2020 February 10 Kwanini Kuna Tafsiri Tofauti kwa Wakristo?

Kwanini Kuna Tafsiri Tofauti kwa Wakristo?

Kwanini Kuna Tafsiri Tofauti kwa Wakristo?

KWA NINI KUNA TAFSIRI TOFAUTI KWA WAKRISTO?

Biblia inasema katika Waefeso 4:4-6 “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”. Maandiko haya yanasisitiza umoja ambao lazima uwepo katika mwili wa Kristo sababu sisi sote tumejazwa na “Roho mmoja”. Pia, Mtume Paulo anatukumbusha tena katika 1 Wakorintho 2:10-13, Roho Mtakatifu anatusaidia kuchunguza mambo yote, hata mafumbo ya Mungu. Swali ni kwamba, pamoja na ukweli huo, kwanini kuna tafsiri nyingi na tena tofauti katikati wa Wakristo?

Katika maisha ya ufuasi wa Yesu, kila muumini analo jukumu kuijua kweli ya Biblia na kuyatumia maandiko kwa haki (2 Timotheo 2:15), kwa maana Roho Mtakatifu yupo teyari kutusaidia. Lakini, si kila mtu ambaye ana Roho Mtakatifu, anamsikiliza au anamwelewa Roho Mtakatifu, kwakuwa kuna ‘wakristo’ wengi ambao wanamhuzunisha Roho wa Mungu, (Waefeso 4:30), kwani hawayatendi mapenzi ya Bwana. Hivyo, sababu moja kubwa ya watu kuwa na tafsiri tofauti ya Biblia ni kwamba baadhi yao hawamsikilizi Mwalimu – yaani Roho Mtakatifu.

Baadhi ya sababu zingine ni kama hizi zifuatazo:

Kutoamini.

Ukweli ni kwamba wengi ambao wanadai kuwa ni Wakristo hawajawahi kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokoka. Wao huvaa nembo ya “Ukristo” lakini hawajakuwa na badiliko la kweli mioyoni mwao. Wengi wao hawaiamini Biblia kwamba ina mamlaka ya kweli na kuifundisha hivyo. Wao wanajinadi kuzungumza kwa niaba ya Mungu wakati bado wanaishi katika hali ya kutoamini.

Ni vigumu kwa mtu asiyeamini kutafsiri maandiko kwa usahihi. “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maan kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni” (1 Wakorintho 2:14). Mtu ambaye hajaokoka hawezi kuuelewa ukweli wa Biblia. Yeye hana ujazo wa roho mtakatifu. Ni vyema tukijua kwamba, hata kuwa mchungaji au msomi wa mambo ya kidini haimwakikishii mtu kuwa na wokovu, isipokuwa amempokea Bwana na kumkiri kuwa Bwana na Wokozi wa maisha yake.

Mfano wa machafuko yaliyotokana na kutoamini hupatikana katika Yohana 12:28-29. Yesu anaomba kwa Baba, akasema, “Baba, litukuze jina lako.” Baba anajibu kwa sauti inayosikika kutoka mbinguni, ambayo kila mtu aliyekuwako karibu alisikia. Lakini kumbuka hata hivyo, kulikuwa na tofauti katika tafsiri: “Umati ambao ulikuwa mahala pale ulisema ulisikia sauti hiyo kama radhi; wengine walidai kuwa malaika alikuwa anaongea naye. Lakini pamoja na watu wale kusikia sauti moja toka mbinguni, ‘bado kila mtu alipata kusikia kile alitaka kusikia’.

Ukosefu wa mafunzo.

Mtume Petro anaonya dhidi ya wale ambao hutafsiri maandiko vibaya. Anahusisha mafundisho yao ya uongo katika sehemu kwa dhana kwamba wao ni “wapumbavu” (2 Petro 3:16). Timotheo anaambiwa kwamba “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15). Hakuna njia ya mkato kwa tafsiri sahihi ya Biblia, sisi tumeamurishwa kujifunza.

Ufafanuzi mmbaya.

Makosa mengi yamekuzwa kwa sababu ya kushindwa kutumia ufafanuzi mzuri kwa kuligawa sawsawa neno la Mungu. Kuchukua mstari nje ya mazingira yake unaweza kuleta uharibifu mkubwa kwa maana halisi ya mstari husika. Kutozingatia mazingira pana ya sura na kitabu (context), au kushindwa kuelewa mazingira ya kihistoria au kitamaduni pia husababisha matatizo katika tafsiri.

Upumbavu wa neno la Mungu.

Apolo alikuwa muhubiri mashuhuri na fasaha, lakini alijua ubatizo wa Yohana tu. Hakuwa anamjua Yesu na namna ya upatikanaji wa wokovu wake, hivyo ujumbe wake ulikuwa haujakamilika. Aquila na Priscilla walimchukua na “kumwelezea zaidi njia ya Mungu kwa undani” (Matendo 18:24-28). Baada ya hapo, Apolo anaonekana anahubiri juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya vikundi na watu binafsi hii leo wana ujumbe ambao haujakamilika kwa sababu wanatilia umakini vifungu fulani na kuvitupilia nje vifungu vingine huku wakishindwa kuzitambua nyakati sahihi za utimilifu wa kusudi la Mungu.

Ubinafsi na kiburi.

Inasikitisha kusema kwamba, tafsiri nyingi za Biblia hivi leo, zinalenga kukidhi haja ya mtu fulani kwa lengo la kutimiza haja zake binafsi na hivyo kuyafanya yawe mafundisho manyonge. Baadhi ya watu huona fursa ya kunufaika kibinafsi na kukuza “mtazamo mpya” katika maandiko. (Angalia maelezo ya walimu wa uongo katika waraka wa Yuda.)

Kushindwa kukomaa.

Wakati Wakristo wengi hawakui na kukomaa kiroho vile iwapasavyo, uelewa wao wa neno la Mungu umeathirika. “Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini.” (1 Wakorintho 3:2-3)

Mkazo usio na maana wa utamaduni.

Baadhi ya makanisa hudai wanaamini Biblia, lakini tafsiri yao daima huchujwa kupitia mila za makanisa yao. Mahali ambapo utamaduni na mafundisho ya Biblia zinahitilafiana, utamaduni hupewa kibao mbele. Hii kwa kwa namna kubwa hupunguza mamlaka ya neno la Mungu na kuyapa mapokeo mamlaka katika uongozi wa kanisa. Ikumbukwe kwamba, katika mambo yote ya muhimu, Biblia iko wazi kabisa katika kila eneo. Hakuna jambo lililoachwa lilete utata kuhusu uungu wa Kristo, hali halisi ya mbinguni na kuzimu, na wokovu kwa neema kupitia imani.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *