Home 2020 February 05 Yasiyosemwa Juu ya Zaka

Yasiyosemwa Juu ya Zaka

Yasiyosemwa Juu ya Zaka

Mpendwa katika Kristo,

Najua ni mara kadhaa umesikia mafundisho juu ya utoaji wa zaka. Lakini, najua kwa hakika hujaambiwa vya kutosha kuhusu zaka. Katika jambo ambalo Mungu hakumpa uhuru Musa afanye atakavyo, ni pamoja na utoaji, upokeaje na utumiaji wa ZAKA! Yapo mengi yasiyosemwa na walimu wa zaka, wale wanaojiita Walawi wa kisasa, moja ya hayo ni maagizo ya Mungu kwa Musa katika Kitabu cha HESABU Sura ile ya 18.

Hapa chini, nimekuwekea mstari wa 20-28, kwa ajiri ya rejea ya hayo ninayosema, ambayo wala zaka wa kisasa, KAMWE hawawezi kukuambia! Acha Biblia ijitetee yenyewe, kwa UTUKUFU WA JINA LA KRISTO YESU!

20 Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli.
21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.
22 Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa.
23 Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.
24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.
25 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
27 Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu.
28 Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.

Author: seta sanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *