Home 2020 February 05 Paulo na Ufufuko wa Kristo

Paulo na Ufufuko wa Kristo

Paulo na Ufufuko wa Kristo

Paulo ni uthibitisho wa ufufuko wa Kristo

Kutokana na kumbukumbu za Kibiblia, Paulo ndiye mtume pekee aliyeitwa na Kristo baada ya kufufuka kwake (1 Timotheo 2:7, Matendo 9:15). Mitume wale kumi na mbili (akiwemo Mathiya) walikuwa ni wanafunzi wa Bwana alipokuwa bado yupo ulimwenguni, kabla ya kifo chake (Matendo 1:21-26). Paulo (alikuwa akiitwa Sauli) hakufanya lolote zaidi ya kupinga huduma ya Bwana kabla na baada ya kifo chake mpaka pale Bwana alipomtokea katika utukufu wa kufufuka kwake. Bila ufufuko wa Kristo, tusingekuwa na Paulo, isipokuwa Sauli. Hii inamfanya Paulo kuwa mtume wa ufufuko wa Kristo.

Paulo na ujumbe wa ufufuko

“Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yetu ni bure“ (1 Wakorintho 15:13-14).

Wakati utume maalumu wa mtume Paulo unapokataliwa, ni dhahiri, kwa maneno au vitendo, kwamba huduma ya Kristo mfufuka, kupita mwili Wake (Kanisa), inakataliwa. Ilikuwa ni Bwana mwenyewe kutoka kwenye utukufu wake, ambaye kwa mara ya kwanza aliweza kufafanua fundisho, mtembeo, na hatima ya kanisa lake. Yote hayo unaweza kuyapata tu katika mafundisho ya mtume wa Kristo mfufuka. Ufufuko wa Kristo haukuwa muhimu kwa kutunza sheria, kujenga ufalme, wala imani yenye kuongeza matendo iliyokuwa ikihubiriwa na wale Thenashara. Mitume kumi na wawili wa huduma ya kifalme ya Israeli waliweza kuhubiri injili yao ya mfalme na ufalme kabla ya Kristo kufa na kufufuka. Hata baada ya ufufuko, wale kumi na wawili walibakia Yerusalemu (Matendo 8:1; 11:19) na baadaye waligeuka na kuwa kundi dogo la watunza sheria waliomkubali Masihi (Matendo 21:20). Mtume wa ufufuko amedai kupokea maagizo aliyopewa kutoka kwa Bwana mfufuka mwenyewe, hakuna mwanadamu angeweza kumfunulia mapokeo yake:

“Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi, kama inenavyo injili yangu” (2 Timotheo 2:8)

“Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele” (Warumi 16:25).

 

Paulo kuhojiwa kwa sababu ya ufufuko

Kuitwa kwa Paulo na ujumbe wake ulisimama juu ya ufufuko.

“Ndugu zangu, … mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu” (Matendo 23:6)

Watakatifu wa Yerusalemu walikubalika kwa sababu ya juhudi yao katika sheria. Haikuwa utume wa Paulo wala ujumbe wake ulioweza kupokelewa, kwa sababu kuukubali ushuhuda wake kungekuwa ni kuyakubali mafunuo ya Kristo mfufuka.

“Kwa nini linadhaniwa kwenu kuwa ni neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?” (Matendo 26:8).

Ushuhuda wa huduma ya Paulo unahitaji uthibitisho wa ufufuko wa Kristo, vinginevyo kuitwa kwake na huduma yake ni uwongo mkubwa zaidi katika Ukristo.

Paulo hakuwa mtume pamoja na wale 12 waliochaguliwa na Bwana katika huduma yake hapa ulimwenguni. Kama Paulo ni mtume wa Kristo, ni ushahidi kwamba Kristo Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.

“Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu); … Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo” (Wagalatia 1:1; 1:20).

Paulo ni udhibitisho wa ufufuko wa Kristo

Kumfuata Paulo ni kumfuata Kristo katika huduma yake ya ufufuko kutoka mbinguni.

Bila ya ufufuko wa Kristo, Paulo hana ujumbe, hana huduma, na hana uokovu, KAMWE NASI PIA!

Kwa UTUKUFU wa Jina lake…

Yesu 100% – Bila Nyongeza

Author: seta sanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *