Je kunatofauti gani kati ya Agano la Kale na Agano Jipya?
Biblia ni kitabu kimoja kinachojumusha Agano la Kale na Agano jipya, kuna tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya japo haya maagano mawili yanakamilishana. Agano la Kale ndio msingi, Agano Jipya linajijengwa kwenye huo msingi na ufunuo zaidi kutoka kwa Mungu. Agano la Kale linanzisha kanuni ambazo zinaonekana kuonyesha ukweli wa Agano Jipya. Agano la Kale lina unabii mwingi ambao unatimia katika Agano Jipya. Agano la kale linatoa historia ya watu wakati lengo la Agano Jipya ni juu ya Mtu.
Agano la Kale linaonyesha ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi wakati Agano Jipya linaonyesha Neema ya Mungu kwa ajili ya wenye dhambi. Agano la Kale linatabiria Masihi (angalia Isaya 53) Agano Jipya linamdhihirisha Masihi kuwa ni nani (Yohana 4:25-26). Agano la Kale linaandika utoaji wa Sheria ya Mungu ambapo Agano Jipya lanaonyesha jinsi Yesu Masihi alivyotimiza sheria hiyo (Mathayo 5:17, Waebrania 10:9). Katika Agano la Kale, Mungu anashughulika hasa na watu wake wateule, Wayahudi; katika Agano Jipya, Mungu anashughulika hasa na kanisa lake mwili wa Kristo (Mathayo 16:18).
Baraka za kimwili zilizo ahidiwa katika Agano la Kale (Kumbukumbu 29:9) zinatoa njia ya baraka za kiroho chini ya Agano Jipya (Waefeso 1:3). Unabii wa Agano la Kale juu ya kuja kwa Kristo ingawa ni wa kina, una kiasi fulani cha utata ambao umerekebishwa/umefafamuliwa katika Agano Jipya. Kwa mfano, Nabii Isaya alisema juu ya kifo cha Masihi (Isaya 53) na kuanzishwa kwa ufalme wa Masihi (Isaya 26) huku hakuna dalili ya mwenendo wa matukio hayo mawili, hakuna mwanga kwamba mateso na ujenzi wa ufalme utatenganishwa na milenia. Katika Agano Jipya, hatahivyo, inakuwa wazi kuwa Masihi atakuwa na ujio wa aina mbili: katika ule wa kwanza aliteseka na akafa (na kufufuka tena), na katika ule wa pili Yeye ataimarisha/kuujenga ufalme wake.
Ufunuo wa Mungu katika maandiko ni endelefu, Agano Jipya huleta kwa uwazi zaidi kanuni zilizowekwa/zilizoletwa katika Agano la Kale. Kitabu cha Waebrania kinaeleza jinsi Yesu kuwa ndiye Kuhani Mkuu na jinsi kafara yake moja ni kuu kupita sadaka zote za awali, ambazo zilikuwa kivuli cha yatakayokuja. Pasaka ya Agano la Kale (Ezra 6:20) inakuwa Mwana-kondoo wa Mungu katika Agano Jipya (Yohana 1:29). Agano la Kale linatupa sheria, Agano Jipya linafafanua kwamba sheria ilikuwa ni maana ya kuwaonyesha watu mahitaji yao ya wokovu na haikukusudiwa kuwa njia ya wokovu (Warumi 3:19).
Agano la Kale lilionyesha jinsi Adamu alivyopoteza paradise wakati Agano Jipya linaonyesha jinsi paradiso inavyopatikana tena kupitia Adamu wa pili (yaani Kristo). Agano la Kale linasema kwamba mwanadamu alikuwa ametengwa na Mungu kwa njia ya dhambi (Mwanzo 3), Agano Jipya linasema kuwa mwanadamu anaweza kurejeshwa katika uhusiano wake na Mungu (Warumi 3-6).
Agano la Kale lilitabiri maisha ya Masihi, injili zimerekodi maisha ya Yesu, na Nyaraka hutafsiri maisha yake na jinsi sisi tunavyotakiwa kuitikia yote ambayo amefanya. Kwa muhtasari, Agano la Kale huweka msingi wa kuja kwa Masihi ambaye atajitoa nafsi yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (1 Yohana 2:2). Agano Jipya linaonyesha huduma ya Yesu Kristo na kisha linaturudisha nyuma kuangalia kile alichofanya na jinsi sisi tunavyostahili kuitikia. Maagano yote mawili humfunua Mungu huyo huyo mtakatifu, wa huruma na haki ambaye analaani dhambi lakini anatamani kuwaokoa wenye dhambi kwa njia ya sadaka ya upatanisho. Katika Maagano yote mawili, Mungu hujifunua kwetu na anatuonyesha jinsi sisi tunavyostahili kwenda kwake kwa njia ya imani (Mwanzo 15:6; Waefeso 2:8).
Leave a Reply