UKUTA TENGANISHI!
Biblia Takatifu inazungumza juu ya ukuta uliowatenganisha wanadamu wote katika sehemu kuu mbili. Katika Waefeso 2, Sheria (Amri Kumi), inaitwa “ukuta wa kati (kiambaza cha kati).”
Sheria walipewa watu wa agano wa Mungu – Wayahudi! Wasio Wayahudi, walikuwa tayari ‘wameshatupwa’ zamani sana, wakati wa Mnara wa Babeli na Mungu alikuwa amemwita (amemchagua) Ibrahimu na uzao wake na kuwapa Sheria. Wateule hao, hata hivyo, walivunja Sheria hizo walizopewa, ndio maana Warumi 3:19 inasema:
“Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu.”
Kwa sababu ya uvunjwaji wa Sheria hiyo, watu wote wamewekwa kwenye kiwango sawa cha uovu; Lakini, hili pia, lilikuwa ni kusudi la Mungu la NEEMA: “Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi, ili awarehemu wote” (Warumi 11:32). Na hivyo Mungu hutoa wokovu kwa watu wote kwa njia ya Kristo, ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu pale Kalvari. Hii ndiyo sababu Waefeso 2:11-22 inasema:
“Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.”
честные казино с быстрыми выплатами
бездепозитные бонусы казино
играть в лучшем казино на деньги
база казино с бездепозитным бонусом
онлайн казино России
casino oyunu
Hatuna budi kumshukuru sana Mungu wetu, kwamba, sasa hakuna tena “UKUTA KIZUIZI”, kati ya MUNGU na wale wanaomtumaini Mwanawe, wala kati ya WAAMINI ambao wamefanywa kuwa “Mwili mmoja katika Kristo.”
Utukufu una Yeye KRISTO YESU Milele na Milele AMINA
Leave a Reply